Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema itaendelea kuhakikisha
miradi ya mazingira katika maeneo mbalimbali nchini inatekelezwa kwa
kiwango kinachotakiwa ili iwanufaishe wananchi na kutatua changamoto za
kimazingira.
Pia, imesema itashirikiana na Wizara nyingine za kisekta kuona namna namna
bora ya kuvuna maji ili kudhibiti mafuriko yanaoyakumbuka maeneo
mbalimbali nchini na kusababisha adha kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis leo Aprili 19, 2023 bungeni jijini
Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Jeremiah
Mrimi.
Katika swali la msingi Mhe. Mrimi alitaka kujua mpango wa Serikali wa
kudhibiti mafuriko katika Mto Mara kwa kuvuna maji yake kupitia mabwawa
na kujenga skimu za umwagiliaji.
Akiendelea kujibu swali hilo Mhe. Khamis amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa
Rais ina utaratibu wa kutembelea na kukagua miradi inayoratibiwa na Ofisi
hiyo na kutoa maelekezo ikamilike kwa wakati na kwa kiwango.
Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imezindua
Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) ambao
umeelezea mikakati na shughuli endelevu zinazoweza kufanyika ili kuhifadhi
mazingira.
“Mheshimiwa Spika, Mto Mara ni moja ya mito mikubwa na muhimu nchini
Tanzania. Hivyo, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara nyingine
za kisekta zitakaa na kuona namna bora ya kuvuna maji ili kudibiti mafuriko,”
amesema.
Mhe. Khamis amefafanua kuwa Serikali itaimarisha usimamizi wa vyanzo vya
maji na kuhakikisha uwepo wa mtiririko wa uhakika katika mito ikiwemo mito
mbalimbali ikiwemo Mara, Kagera, Ruaha Mkuu, Momba, Lufurio, Wami na
Ruvuma.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema pia Serikali itahamasisha matumizi sanifu
kwa watumiaji wote wa mito hiyo pamoja na kuimarisha viwango vya