Mdhamini wa Mshindano ya Tambaza Ramadhani Cup ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Michezo Wilaya ya Ilala Chama Cha Mapinduzi (CCM) Imran Baba akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu wanaoshiriki Mashindano ya Tambaza Ramadhani Cup pamoja na viongozi wa CCM Kata ya Jangwani.
…………………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Timu ya Umoja imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Mashindano ya Tambaza Ramadhani Cup baada ya kuitoa timu Twariqa kwa mikwaju ya penati 6 kwa 5 katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliochezwa leo tarehe 18/4/2023 katika Uwanja wa Fire, Jijini Dar es Salaam.
kufatia matokeo hayo Timu ya Umoja itaminyana na Mikumi katika hatua ya fainali katika mchezo ambao umepangwa kupigwa siku ya Alhamisi ya tarehe 20/4/2023 katika Uwanja wa Fire uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mdhamini wa Mshindano ya Tambaza Ramadhani Cup Imran Baba, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutoa elimu kuhusu maadili pamoja na kukuza vipaji vya vijana.
“Michezo ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku, tuendee kuwa na upendo, nitaendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya viwanja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali” amesema Imran Baba.
Mratibu wa Mashindano ya Tambaza Ramadhani Cup Awadhi Dinongo, amesema kuwa mashindano yanaendelea vizuri, huku akieleza kuwa mshindi wa kwanza anatarajia kupata Ng’ombe, jezi na kikombe, mshindi wa pili atapata Mbuzi na kikombe na mshindi wa watatu atapata jezi, mpira pamoja na kikombe.
“Tunamshukuru mdhamini wetu Imran Baba kwa ushirikiano wake mkubwa, pia tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Fainali katika mashindano Tambaza Ramadhani Cup yanatarajia kuchezwa tarehe 20/4/2023” amesema Dinongo.
Michuano ya Tambaza Ramadhani Cup imeshirikisha timu 10 kutoka Kata ya Jangwani ambapo yanatarajia kufikia tamati siku ya Alhamisi.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Mjumbe wa Kamati ya Michezo Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Bw. Imran N. Jaffer maarufu kwa Jina la Imran Baba.