Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitafa mwaka 2023,Abdalla Shaib Kaim akipanda mti ishala ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kuhimizana wananchi kupanda miti kadri wawezavyo.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitafa mwaka 2023,Abdalla Shaib Kaim akipanda mti ishala ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kuhimizana wananchi kupanda miti kadri wawezavyo.
…………………………
Na Fredy Mgunda, Iringa.
ZAIDI ya miti 600 rafiki na maji imepandwa katika chanzo cha maji cha Ruponda katika Kijiji cha Ruponda kata ya Ruponda kwa ajili ya kulinda mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa ajili ya faida ya sasa na vizazi vijavyo.
Miti hiyo imepandwa wakati mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 zilizokuwa zinakimbizwa katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa lengo la kutunza na kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji ili kulinda mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha viongozi wa Mwenge wa Uhuru na WANANCHI wa kata ya Ruponda kupanda miti rafiki na maji, Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa chanzo hicho cha maji kitaendelea kutunzwa miaka yote kama ambavyo kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inavyotaka kuhifadhi vyanzo vya maji.
Moyo alisema kuwa uongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea itaendelea kutunza mazingira na vyanzo vya maji kama ambavyo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Philipo Mpango alivyoagiza kila wilaya kupanda miti kulingana na ukubwa wa eneo.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitafa mwaka 2023,Abdalla Shaib Kaim aliupongeza uongozi wa serikali ya wilaya ya Nachingwea kwa upandaji miti na kuwataka waendelee kupata miti kila wakati.
Kaim aliwataka Wananchi na viongozi wa wilaya ya Nachingwea kuhimizana kupanda miti kwa lengo la kulinda vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.