Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo April 14 amefuturisha Mamia ya Wananchi wa Mkoa huo katika Futari iliyohusisha viongozi na wawakilishi wa makundi mbalimbali Katika jamii.
Akizungumzia wakati wa Hafla hiyo iliyofanyika Viwanja vya Karimjee, RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kudumusha umoja wa kidini uliopo baina ya wakristo na Waislamu.
Aidha RC Makalla ametumia hafla hiyo kumtangaza Sheikh Walid Alhad Kawambwa ambae ni Kaimu Sheikh wa Mkoa huo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo na kutoa wito kwa Wananchi kumpatia ushirikiano Ili kuendelea kudumusha amani.
Kwa Upande wao baadhi ya Wananchi waliopata fursa ya kushiriki hafla hiyo wamemshukuru RC Makalla kwa mwalio na heshima kubwa aliowapatia na wameahidi kuendelea kushirikiana nae katika masuala mbalimbali.
Futari ya Mkuu wa Mkoa imehusisha Wananchi wa makundi yote wakiwemo Viongozi wa kiserikali, viongozi wa Dini zote, Viongozi wa Taasisi, Machinga, Bodaboda, Yatima, Wajane, Wenye ulemavu na wasiojiweza na wadau wengine.