Na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Polisi Jamii kitengo cha Ushirkishwaji wa Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma leo tarehe 15, 2023 limeendelea na kutoa elimu kwa umma juu ya kupambana na kuporomoka kwa maadili katika Jamii kupitia vyombo vya habari katika viunga vya Hotel ya Royal Village iliyopo Jijini Dodoma.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limesema linamikakati mingi ya kupambana na kuzuia Uhalifu kama vile ‘Familia yangu haina mhalifu, kuanzisha Mradi wa Polisi kata kwa kila kata pamoja na Uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi na kuitaka jamii kushirikiana vyema na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za Uhalifu na Waalifu.
Pia Jeshi la Polisi limezitaka Familia za Kitanzania kurejesha Maadili katika jamii kwa kuanzia ngazi ya familia, pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazopambana na kuporomoka kwa maadili kama vile Jeshi la Polisi.
Watoaji wa Elimu hiyo ni Mrakibu wa Jeshi la Polisi SP Daktari Ezekieli Kyogo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Dotto Manase, Wasanii kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Staffu Sajini wa Polisi Manjinja Ndolela na Koplo wa Polisi Salum a.k.a Mr Finest