Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadili suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya Plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadili suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya Plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Mnkunda akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadili suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya Plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wadau mbalimbali wakishiriki katika mkutano huo.
Kuwepo kwa kelele mtaani kutoka kwenye baadhi kumbi ya starehe na makanisa imekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi kutokana na kelele zinazokithiri kwenye makazi ya watu jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Wamiliki wa kumbi hizo, viongozi wa dini na watendaji wa serikali za mitaa kwenye mkutano ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Amoss Makalla amesema kelele mitaani imekuwa changamoto na anapata malalamiko kutoka kwa wananchi huku baadhi yao wakiwa wanatuma sauti za kelele hizo kutumia simu zao na kulalamika kwa kiongozi huyo.
Kero imekuwa kubwa sana na imebidi mkuu wa mkoa kukutana na Wamiliki wa kumbi za starehe na makanisa kuongea nao katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ili kuona namna ya kutatua kero hizo ambapo amewasihi kufuata taratibu na sheria ziliwekwa ambazo zimethibitishwa na NEMC na kufuata sheria ziliwekwa kwenye leseni zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amesema bado changamoto ni kubwa japo wamejitahidi kufanya namna mbali mbali za kutatua changamoto hizo lakini wameona ni vyema leo kuwakutanisha viongozi wa dini, watu wenye kumbi za starehe pamoja na watendaji wa serikali za mitaa kujadili upya changamoto hizo ili waone namna bora ya kuzitatua.
Hata hivyo leo kwenye mkutano huo walikuwepo watengenezaji na wasambazaji wa vifungashio ambapo ilitolewa elimu kwa wahusika hao ili kupata maoni kwao na kujua changamoto wanazokutana nazo.
Mifuko ya Plastiki imeonekana kurudi mitaani kwa njia ya vifungashio na kusababisha uchafusi wa mazingira hivyo mkurugenzi wa Baraza la mazingira Nemc awasihi watendaji wa serikali za mitaa kufuatilia mitaa yao na kuhakikisha viwanda hivyo ambavyo vishakatazwa kusitisha haraka uzalishaji wa mifuko hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Mnkunda amesema katika hatua ya kuhakikisha wanasafisha na kupendezesha mkoa wa Dar es salam yeye kushirikianana na viongozi wa mitaa husika watahakikisha wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi kumuunga mkono Mkuu wa mkoa Amoss Makalla.
“Sisi viongozi wa wilaya husika tupo tayari kushiriki na NEMC katika kutatua changamoto zinazokabili wananchi katika Wilaya zetu,”.Amesema Mwanahamisi Mnkunda