Katibu
Tawala Mkoa Bw. Ally Senga Gugu ameongoza wakazi wa Dodoma katika katika
mapokezi ya Mabingwa wa Shule za Sekondari Afrika (CAF) Fountain Gate
walioiwakilisha Tanzania na Ukanda wa Afrika mashariki (CECAFA) katika
mashindano ya Shule za Sekondari yaliyofanyika Durban, Afrika Kusini. Mapokezi hayo
yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Fountain Gates Bw. Japhet Makau akizungumza
katika hafla ya mapokezi ya Timu ya mpira wa Miguu ya wasichana mara baada ya
kuwasili jijini Dodoma. Katika mashindano hayo
timu ya Fountain Gate imejinyakulia kitita cha Dola za Marekani 300,000 pamoja na kombe.
Kikosi
cha ushindi cha timu ya Fountain Gate mara baada ya kupokelewa na Katibu Tawala
wa Dodoma Bw. Ally Gugu (hayupo pichani) katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.
………………
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu ameshiriki katika mapokezi ya Mabingwa wa Shule za Sekondari Afrika (CAF) Fountain Gate walioiwakilisha Tanzania na Ukanda wa Afrika mashariki (CECAFA) katika mashindano ya mpira wa Miguu kwa wasichana ngazi ya Shule za Sekondari yaliyofanyika Durban, Afrika Kusini.
Mapokezihayo yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma ambapo
shule mbalimbali zilikusanyika na viongozi wa Serikali kwa ajili ya mapokezi ya
Mabingwa hao.
“Sisiwenzenu wa Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote
za Mkoa wa Dodoma tuna furaha sana na tunawashukuru wenzetu wa Fountain Gate
kwa kutuheshimisha na kutupa furaha hii na pengine ni kama vile sisi tulijua
dhamira yenu na kazi kubwa ambayo mmewekeza katika kuwajenga vijana hawa
wa wakiume na kike katika kushiriki mashindano siyo tu ya Mkoa bali ngazi ya
Kitaifa na Mataifa
“Nakumbukakabla ya kwenda kwenye mashindano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilipata fursa ya kuwakaribishapale Mkoani tulikutana na tulifurahi tukapata chakula cha pamoja na sisi kamawatumishi wa Mkoa huu tumeona baraka wa lile ambalo Mkuu wa Mkoa
alilifanya kwasababu baada ya kuwaaga vizuri kwa kuwapa tuzo na hamasa ambayo
Mkoa ulifanya tunawashukuru sana kwa kubeba dhima ile na kuenda kuifanyia kazi
leo hii mmekuja kutufurahisha kwa kweli tunawashukuru sana na kuwapongeza kwa
dhati. ” Amesema Gugu
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Fountain Gates Bw. Japhet Makau amewashukuru wana Dodomakwa mapokezi mazuri kwani ni nje ya matarajio yao na kuelezea namna walivyoibukawashindi.
“TumetokaDurban, Afrika Kusini ambapo mabinti zetu timu ya Sekondari ya Wasichana ya
Mpira wa miguu Fountain Gate wamekuwa mabingwa wa soka wa Afrika kwa shule za
Sekondari, mashindano haya yalianza ngazi ya shule ambapo katika Tanzania shule
za Mkoa wa Dar-es-Salaam na Tanga zilishirikishwa lakini sisi tuliomba
kushiriki kwasababu muda ulikuwa ni mfupi na sisi tukaibuka kuwa washindi
“Tulienda kuiwakilisha Tanzaniakatika mashindano ya CECAFA ambapo tulijinyakulia Millioni Mia Mbili zaKitanzania kama washindi wa michuano hiyo sambamba na kombe baada ya hapotukakakiwa kwenda Afrika Kusini ambapo kulikuwa na zaidi ya Mataifa 11 lakinikatika timu za wasichana zilikuwa timu sita katika mashindano ambapo mechi ya
kwanza tulipangwa kucheza na wenyeji Afrika Kusini na Fountain Gate ilishinda
goli 7 kwa moja, mechi ya pili Gambia na Fountain Gate, nusu fainali goli nne
kwa sifuri tukapata tiketi ya kucheza fainali na Morocco ambapo alipata
kichapo cha goli tatu kwa sifuri kwa hiyo timu ya Fountain Gate kutoka
Dodoma wakawa Mabingwa kutoka Tanzania sambamba na ubingwa tuliweza
kupata mchezaji bora, mfungaji bora na goal keeper bora “Amesema Bw. Makau
Katika mashindano hayo timu ya
Fountain Gate imejinyakulia kitita cha Dola za Marekani 300,000 pamoja na kombe.