Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kwimba katika eneo la Hungumalwa wakati akiwa ziarani mkoani Mwanza leo tarehe 11 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Misungwi akiwa ziarani mkoani Mwanza leo tarehe 11 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza changamoto mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Misungwi akiwa ziarani mkoani Mwanza leo tarehe 11 Aprili 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema serikali itawachukulia hatua wale wote watakaobainika wamefanya ubadhirifu wa fedha za umma waliotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliotolewa hivi karibuni.
Makamu wa Rais amesema hayo alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Kwimba akiwa eneo la Hungumalwa wakati wa ziara yake mkoani Mwanza leo tarehe 11 Aprili 2023. Amesema kila kiongozi anapaswa kuhakikisha fedha zinazopelekwa katika eneo lake zinatumika kama ilivyokusudiwa na kukamilisha kwa miradi kwa wakati.
Makamu wa Rais amewataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanaitunza miradi inayopelekwa na serikali ili iweze kudumu kwa muda mrefu. Aidha amewasihi kujikita katika ufugaji wenye tija na utakaowapa matokeo ya haraka ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ufugaji wa kuhamahama.
Akiwa Wilayani Misungwi, Makamu wa Rais amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda na kudumisha amani pamoja kuzingatia maadili ya kitanzania kwa kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yasiofaa kwenye televisheni. Aidha Makamu wa Rais amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanafanikisha watoto wao kupata elimu na kuachana kukimbilia katika shughuli za migodini. Pia amewasihi kuzingatia masuala ya lishe ili kuwa na taifa lenye nguvukazi yenye afya njema.