Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mchungaji Mstaafu Richard Hananja wakati wa uzinduzi wa bonanza la mpira wa miguu lenye lengo la kuhamasisha uchangiaji damu lililoasisiwa na Mwandishi wa habari Anjela Seth kutoka fullShangwe Blog ambapo amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa kuhamasisha jamii kuchangia damu.
Kwa upande wao Afisa uhamasishaji jamii kutoka mpango wa Taifa wa damu salama Fatuma Mjungu na Joyce Jackson kutoka kitengo cha damu salama hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamezungumzia umuhimu wa uchangiaji damu na sifa za watu wenye uwezo wa kuchangia damu
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi hilo ambae ni Mwandishi wa habari Anjela Seth amezungumzia namna ambavyo jamii inapaswa kuhamasishwa kuhusu suala la uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa
Hata hivyo baadhi ya wadau walioshiriki Uzinduzi huo wamepongeza zoezi hilo na kusema kuwa litasaidia kunusuru maisha ya wagonjwa na wameahidi kushiriki zoezi hilo
Bonanza hilo la uchangiaji damu linatarajia kufanyika Mei 6 mwaka huu kwenye kata ya Wazo Mtaa wa mivumoni ambapo mgeni rasmi atakuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt Rashid Mfaume