MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni kushoto akizungumza na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi wakati alipofika kwenye hifadhi hiyo kuitembelea ikiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Hifadhi hiyo na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu
Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi kulia akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni wakati wa ziara yake kwenye hifadhi hiyo
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni katika akiwa ni Meneja wa Benki ya CRDB wilaya ya Same kulia
Watalii wakifurahia utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Tembo akiwa na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi
Na Oscar Assenga aliyekuwa KILIMANJARO
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni ametangaza vita mpya baada ya kuwatahadharisha majangaili ambao wanafikiria kupitia ujangili wanaweza wakanufaika kuachana na biashara hizo kutokana na kwamba wao wamejipanga kuhakikisha wanawashughulikia vilivyo.
Vita hiyo aliitangaza mwishoni mwa wiki wakati alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ikiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani ambapo alisema watahakikisha wanashughuliwa ili kuhakikisha hawagusi hifadhi ikiwemo kuwataka wajiandae kutafuta kazi nyengine .
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kama walifikiria hiyo ndio ajira yao wajiandae kutafuta kazi nyengine kwa sababu yenye ni mhifadhi na anafahamu umuhimu wa hifadhi na ndio Mwenyekiti wa Kamati ya usalama wa wilaya hiyo.
“Hifadhi nyingi zimekuwa zikikabiliwa na vitendo vya ujangili hivyo sisi kama Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya tumejipanga kuhakikisha tunashirikiana na hifadhi kutokomeza ujangili mikakati hiyo ni pamoja na tunapokuwa kwenye mikutano yao ya vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo miongoi mwa mambo tunaowaeleza ni umuhimu wa hifadhi na athari za kuwa na ujangili”Alisema
Mkuu huyo wa wilaya wanapokuwa kwenye ziara katika vijiji hivyo wanawaelimisha wananchi umuhimu wa hifadhi na kuwaonya waache kufanya biashara za ujangili kwa sababu wanapoendelea kuifanya serikali kupitia vyombo vyake itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria.
“Kwa sababu wanakuwa kama wahujumu uchumi kutokana na kwamba hifadhi hizo zinafanya uchumi wa nchi unaweza kuimarisha hivyo kunapokuwa na majangili wanaoua wanyama ambao watalii wanakuja kuangalia hiyo ni hujuma hivyo serikali ya wilaya tumejipanga vizuri kushirikiana na hifadhi kuhakikisha havijitokezi”Alisema Mkuu huyo wa wilaya
Alisema kwamba Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ndio Hifadhi muhimu kwa Kanda ya kaskasini na kuna wanyama wengi wanaopatikana kwenye hifadhi nyengine nchini lakini ukifika eneo hilo una uhakika kuweza kumuona mnyama Faru kiurahisi sana na imesaidia wilaya ya sama kuwa na watalii wengi wanaokwenda kumuona mnyama huyo.
Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu amefanya mambo makubwa sana kupitia Royal Tour imewasaidia sana hifadhi kutokana na kwamba baada ya ziara hiyo wataalii wanaoingia kwa mwaka kwenye hifadhi hiyo kwa sasa ni zaidi ya 7000 hiyo ni faida kubwa walioipata kupitia ubunifu huo.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba Rais Dkt Samia Suluhu kupitia Fedha za Tozo na Fedha za Covid ameweza kuimarisha miundombinu ya hifadhi nchini ambapo miongoni mwa hifadhi ambazo zimenufaika ni mkomazi ambapo kuna majengo ya utawala na barabara nzuri ambao zinahamasisha watalii hivyo Rais amekuwa mfano nzuri wa uhifadhi nchini.
Aidha pia alisema wanapokuwa na hifadhi inayofikika kirahisi wanapata watalii wengi ambazo wanasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu
Hata hivyo aliwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za hapa nchini ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo kuwataka pia wananchi wa wilaya ya Same watumie wikiendi zao kuweza kufika mkomazi kuweza kuona vivutio vilivyopo na hivyo kusaidia serikali kuingiza mapato ambayo yatasaidia maendeleo kwenye wilaya yao.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Utalii wa Hifadhi wa Taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kutokana na kupelekea fedha za Uviko ambapo waliweza kuzitumia kujenga lango maalumu ambalo ni la kuingilia wageni wanaofika kutembelea hifadhi hiyo na kuweza kupata huduma nzuri za utalii.
Alisema kwamba kupitia fedha hizo wameweza kujenga barabara nzuri yenye utefiu wa zaidia ya kilomita 140 na pia kutengeneza viwanja vya ndege na hiyo imetoa fursa kwa wageni ambao hawana muda wa kutembea kwenye magari kwa muda mrefu wakati wa safari zao kutoka maeneo mbalimbali kwenda kuitembelea hifadhi hiyo
Happiness alisema kwa kujengwa uwanja huo kumesaidia wageni kusafiri kutumia ndege kufika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi moja kwa moja kutoka kwenye viwanja vyengine