Waziri wa Habari, Mawasilian0 na Teknolojia ya habari Mh. Nape Nnauye akizungumza wakati wa Tamasha la pasaka lililoandaliwa maalum kwa wajili ya kuombea nchi na kumshukuru mungu kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutimiza miaka miwili akiwa madarakani, tamasha hilo lilifanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
…………………………………………………
Akizungumza jana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye ambaye alimwakilisha Rais wa Tanzania Samia suluhu Hassan katika tamasha la Pasaka amesema mapenzi ya jinsi moja hayana nafasi Tanzania
.
‘Taifa litasimamia maadili ya nchi yetu pamoja tamaduni zetu na nchi itaendeshwa kwa katiba hivyo basi hatutaruhusu mapenzi ya jinsia moja hapa nchini na msimamo upo wazi wala hawaitaji kumumunya Maneno’ Amesema Waziri Nape
Ameongeza kwamba kuruhusu mapenzi ya jinsia moja hapa nchini nikuruhusu laana hivyo Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais Samia suluhu Hassan haitoruhusu kufungua milango ya Laana hapa Tanzania.
Hata hivyo Waziri Nape amesema Rais anawashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kumuombea na kuliombea Taifa kwa ujumla.
Aidha Waziri Nape amesema Rais Samia hataki kodi za dhuluma wala uonevu kwa wananchi na tayari ameunda tume ya kuchunguza haki jinai ili wale wananchi wanaobambikiwa kesi , waliodhulumiwa na kuteseka waweze kupata haki zao pia kuwepo na maridhiano ya amani.
Askofu Mtume Boniface Mwamposa wa Kanisa la “Rising and Sshine” akiongoza maombi kwa ajili ya kuombea taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili akiwa madarakani.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mh. Nape Nnauye pamoja na maaskofu wa makanisa mbalimbali wakishiriki katika maombi hayo yaliyoongozwa na Askofu Mtume Boniface Mwamposa kwenye viwanja ya Leaders jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Richard Hananja akitoa neno katika tamasha hilo.
Mwimbaji Upendo Nkone akitumbuiza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mh. Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Upendo Nkone wakati akitumbuiza katika tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye akashusha burudani kali sana kwa nyinbo zake nzuri.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akakumbushia nyimbo zake kama Malebo na nyingine ilikuwa ni burudani sana.
Mwimbaji Christopher Mwahangila naye hakuwa nyuma alifanya mambomakubwa jukwaani.
Maelfu ya watu waliohudhuria katika tamasha hilo wakipata burudani.
Mwimbaji Emmanuel Mgogo akakiwasha na nyimbo zake mbili zilizowafanya mashabiki wake wasimame wakati wote alipokuwa akitumbuiza.
Mwimbaji Emmanuel Mgogo akakiwasha na nyimbo zake mbili zilizowafanya mashabiki wake wasimame wakati wote alipokuwa akitumbuiza.