Na Masanja Mabula, PEMBA
KANISA la Tanzania Assembles of God (TAG) Kisiwani Pemba limeikabidhi. Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba madarasa sita ya Skuli ya Msingi Makangale baada ya kufanyiwa ukarabati Mkubwa kupitia shirika la Youth With Mission Kilimanjaro na kugharimu zaidi yaa shilingi millioni kumi na tisa (19).
Ukarabati huo umejumuisha Kazi ya kuezeka madaraka matano pamoja na Ofisi ya walimu sambamba ya kupaka rangi madarasa mengine zaidi ya skuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib akizungumza baada ya kupokea madarasa hayo amelishukuru Kanisa Hilo kwa najitoleo yake ya kusaidia sekta ya elimu
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameitaja mnyororo wa taasisi zinazopaswa kushirikiana kuinua kiwango Cha Elimu katika skuli hiyo ambazo ni wazazi ,walimu pamoja na viongozi wa serikali ya Wilaya na Mkoa
Alisema serikali inaridhishwa na hi insi Kanisa hilo linavyosaidia huduma za kijamii na kusema wataendelea kuunga mkono pamoja na kuzithamini juhudi hizo.
“Tunatambua Kazi zinazofanywa na Kanisa hili ni za kupigiwa mfano ,hivyo serikali ya Mkoa inaridhishwa na jinsi mnavyoshiriki kutatua changamoto za wananchi hivyo tunaendelea kuzithamini”alisema.
Mapema Mkurugenzi wa Shirika hilo Terevael Nassar alisema wataendelea kuunga mkono serikali katika kusaidia utatuzi wa changamoto za Jamii.
Alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo wamekuwa wakiitoa katika skuli hiyo lengo ni kuunga juhudi za serikali katika kuboresha Mazingira ya upatikanaji wa elimu.
“Tunaridhishwa mno na Kasi ya. Maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya nane ,hivyo naasisi Kama taasisi hinafsi tunaahidi kuendelea kuziiunga mkono kwa kutoa Misaada pale Hali inaporuhusu”alifahamisha.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amani Pemba Tarehe Khamis Hamad alisema madarasa hayo yatakwenda kumaliza changamoto ya wanafunzi ya kuingia mm mikondo miwili.
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wananchi wa kijiii hicho Kassim Hamad Khamis alisema jamii itaongeza ushirikiano na walimu ili kuleta mabadiliko chanya ya kitaaluma .