Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu mashine zilizopo kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi wakati waliotembelea katika hospitali hiyo ili kuona maboresho mbalimbali yaliyofanywana Bohari ya Dawa katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
………………………………………….
NA JOHN BUKUKU-DODOMA
Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma imeendelea kuimarika baada kuweka mashine tatu za X – ray pamoja na CT Scan ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa ajili ya matibabu ambapo awali wagonjwa walikuwa wanakwenda nje ya mkoa huo kutafuta matibabu.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kikao kazi Cha Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) kilichofanyika kwa siku mbili mkoan humo, Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza, amesema kuwa uwepo wa huduma ya X- ray hizo na CT Scan katika hospital hiyo imesaidia wagonjwa kutibiwa kwa wakati.
Dkt. Ibenza amesema kumekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospital ya rufaa na kupata huduma bora zaidi ya ilivyokuwa huko nyuma
“Kuna idadi ya wagonjwa wengi wanaopata matibabu, kwetu sisi tunaona mapato yanaongezeka baada ya kwenda hospital ya Taifa ya Muhimbili sasa wanakuja kwetu” amesema Dkt. Dkt. Ibenza.
Dk. Ibenza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake ya awamu ya sita kwa jinsi ambavyo amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya maboresho mbalimbali katika huduma za afya kwenye hoapitali hiyo ambayo ni muhimu mkoani Dodoma kwakuwa sasa mkoa huo ni makao makuu ya nchi’
Ameishukuru pia Bohari ya Dawa (MSD)kwa ushirikiano wanaotoa kwa hospitali hiyo kwakuwa kila dawa na vifaa tiba vinavyohitajika vinafika kwa wakati hivyo kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zingeweza kujitoKeza kwa wagonjwa wanaohudumiwa katika hospitali hiyo.
Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu huku wachambuzi wa maabara wakiendelea na kazi na wengine wakimsikiliza wakati wahariri waliotembelea katika hospitali hiyo ili kuona maboresho mbalimbali yaliyofanywana Bohari ya Dawa katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu mashine za X Ray zilizofungwa katika hospitali hiyo wakati waliotembelea ili kuona maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Bohari ya Dawa katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari vitanda maalum pamoja na mashine zilizopo kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi wakati wahariri hao waliotembelea katika hospitali hiyo ili kuona maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Bohari ya Dawa katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Daktari Bigwa wa Mifupa na Ajali, Dkt. Ernest Ibenza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari katika maabara ya kati yenye uwezo wakupima magonjwa yote wakati waliotembelea katika hospitali hiyo ili kuona maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Bohari ya Dawa katika hospitali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.