BAADHI ya wananchi wametoa pongezi kwa Mwenyekiti CCM Mkoa wa wa Iringa, Daud Yassin na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas kwa kazi wanayofanya hasa kwa kuwa karibu na makundi ya vijana wa bajaj, bodaboda na wamachinga.
Wakati Mnec Asas akipongezwa kwa kutoa Sh100 Milioni kwa machinga, Mwenyekiti Yassin ameahidi kusapoti leseni 100 kwa madereva wa 100 watakaojitokeza kupata mafunzo.
Mbali na hayo, viongozi hao wamefanikiwa kuwa karibu na makundi mbalimbali kwenye jamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema viongozi hao wanafanya kazi nzuri sana kwa kuwa karibu na makundi hayo muhimu ya vijana.
Wamewataka waendelee kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa makundi hayo.
Wamesema ukiangalia kwa makini katika makundi hayo, idadi ya vijana ni kubwa.
“Viongozi wengi huwa hawakutani na makundi haya muhimu niwapongeze viongozi hawa wa CCM kwa kazi hii kubwa,tunaomba waendelee kuchapa kazi,” amesema Ajuae Johanes, bodaboda wa Kituo cha Kihesa.
Kwa upande wake, Anitha Lucas mkazi wa Mkimbizi amesisitiza viongozi hao kuendelea kuchapa kazi.