…………………….
WAKULIMA wa zao la mpunga Wilayani Kilosa Tarafa ya Kimamba wameiomba serikali kuingilia kati kufukuza ndege aina ya kweleakwelea waliovamia mashamba yao na kula mazao hayo wakati huu wa msimu wa kilimo.
“Tunaomba serikali iingilie kati maafa haya kwa kupuliza dawa ili ndege hawa wasilete madhara zaidi katika mashamba yetu”Wakizungumza na mwandishi wa habari katika Tarafa hiyo wamesema zaidi ya ekari 300 zimevamiwa katika vijiji vya Kimamba A na B pamoja na maeneo jirani ya Tindiga, Kilangali na Ngaite,
Akizungumzia sakata hilo mwenyekiti wa wakulima hao Sadallh Nakitepe amesema idadi ya ndege waliovamia haijulikani lakini wanazaliana kwenye mapori jirani ya mashamba hayo na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka ili kunusuru mazao yao Kondo Shaabani amesema maafisa wa kilimo kutoka ngazi ya Mkoa wamefika na kufanya tathmini ya athari lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ili kunusuru mazao yao
“serikali ifike haraka ili tupate kusaidiwa, tumekopa katika mabenki ili kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga lakini angalia ndugu Mwandishi hali ilivyo hapa shambani, hakuna mazao”
Alisema Katika siku za hivi karibuni Kilimo cha zao la mpunga kimezidi kushika kasi katika Wilaya ya Kilosa ambapo wakulima wanalalamikia gharama za kulimia ikiwa ni pamoja na kukodi mashamba, kuandaa mbegu pamoja na kulinda madhara ya ndege wasivamie mashamba katika vijijiNaye
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bi. Elina Dastan amesema wameshafanya mazungumzo na wakulima kwa nyakati tofauti na kukubaliana kusubiri ndege serikalini ili dawa ipulizwe katika mashamba, hivyo wakulima wawe watulivu wakati huu wanaposubiri ndege hiyo.
Pia afisa huyo ameshauri wakulima kuwekeza katika Bima za mazao kutokana na majanga makubwa kama haya ya kuvamiwa na ndege au wadudu kwenye mazao