Wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika mashindano ya shule za Sekondari Afrika Fountain Gate Dodoma High School wamefanikiwa kushinda mchezo wa Fainali dhidi ya timu ya wasichana yay a mpira wa miguu ya Ecole Omar IBN Khatab kutoka Morocco kwa magoli 3-0.
Timu ya Fountain Gate imetwaa taji hilo kwa upande wa Wasichana katika Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) hatua inaiyoiwezesha kuvuna kitita Cha Dola za Marekani 300,000 sawa na Shilingi Milioni 697 kama Mabingwa wa mashindano hayo Afrika katika Fainali hizo zilizoshuhudiwa pia na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, (Mb), aliyeiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Awali kabla ya kutinga hatua ya Fainali wawakilishi hao wa Tanzania Timu ya shule ya Wasichana ya Fountain Gate mapema leo April 8 2023 ilishuka dimbani dhidi ya timu ya wasichana ya Csg De Mfilou kutoka nchini Congo na kuifunga magoli 4-0.
Viongozi wengine walioshuhudia mashindano hayo yaliyofanyika Durban nchini Afrika Kusini ni pamoja na viongozi mbalimbali wa mpira Afrika wakiongozwa Rais wa Shirikisho la mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe, Mawaziri wa Michezo kutoka nchi washiriki wa mashindano hayo na Tanzania ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma na Rais wa TFF, Wallace Karia