Muonekano wa zahanati ya Mwanalugali A, Halmashauri ya Mji Kibaha,Pwani iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF ,ambayo ujenzi wake imekamilika kwa kwa asilimia 95.
……………………………..
Na.Mwandishi Wetu,Kibaha.
Ujenzi wa mradi wa Zahanati ya Mwanalugali A Kibaha Mjini unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF itakayowahudhumia wakati 3367 umefikia asilimia 95
Katika kufanikisha ujenzi wa mradi huo,jumla ya wananchi 1009 wamejitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutoa nguvukazi ili kupunguza gharama za ujenzi na kuharakisha ukamilishaji ambapo jumla ya Shilingi 22,000,000 zimeokolewa kwa nguvukazi yao
Mratibu wa TASAF Kibaha Mjini Anitha Lyoka amesema kando ya kufikia 95% mradi haujanza kutumika kwani fedha za ujenzi zimeisha
“Fedha ya ujenzi imeisha na ujenzi bado haujafikia 100%,taratibu za kuomba fedha kutoka TASAF makao makuu kwa ajili ya ukamilishaji zinaendelea”ameongeza
Diwani wa Kata ya Tumbi kwenye Mtaa Mtaa wenye mradi Mhe.Raymond Chokala ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo unaolenga kuimarisha afya za Wananchi na kuwa huo ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema yeye kama msimamizi wa Halmashauri anaendelea kutekeleza wajibu wake kuhakikisha thamani ya fedha inaendana na ubora wa miundombinu inayotekelezwa
Gharama ya mradi ni shilingi milioni 113,964,285 kati ya fedha hizo TASAF imetoa shilingi 91,964,285 na mchango wa Jamii ni shilingi 22,000,000