Meneja Mipango ,Tathmini na Ufuatiliaji wa Bohari ya Dawa MSD Hassan Ibrahim akiwasilisha mada Katika kikao kazi kati ya wahariri na Bohari ya Dawa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bw.Tukai Mavere akiandika maswali aliyokuwa akiulizwa na wahariri hawapo pichani wakati wa kikao kazi kiilichokua kikiemdelea kwenye ukumbi wa Tume ya Uchaguzi jijini Dodoma, kulia ni Mwenyekiti wa Kikao hicho Mhariri wa gazeti la Habari Leo Bw. Mugaya Kingoba.
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Bohari ya Dawa Bi. Etty Kusiluka akiweka sawa jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile kabla ya kuwasilisha mada yake kuhusu waandishi WA habari wanavyoweza kuisaidia kutangaza Bohari ya Dawa MSD.
Baadhi ya wahariri wakishiriki Katika kikao kazi hicho kati ya wahariri na MSD.
……………………….
Bohari ya Dawa MSD imesema imeamua kuanzisha Viwanda vya kuzalisha Dawa Ili kurahisisha huduma za kiafya katika hospitali, vituo mbalimbali vya Afya na zahanati nchini.
Meneja Mipango ,Tathmini na Ufuatiliaji wa Bohari ya Dawa Hassan Ibrahim ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada Katika siku ya pili ya kikao kazi kati ya wahariri na Bohari ya Dawa ili kuwajengea ufahamu namna bohari hiyo inavyofanya kazi zake, Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Uchaguzi House jijini Dodoma kikiwashirikisha pia waandishi habari Kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Ibrahim amesema Viwanda vinavyotengenezwa na MSD ni pamoja kiwanda cha barakoa kilichopo Keko Dar es salaam,Kiwanda Cha mipira ya Mikono Cha Gloves ambacho mpaka sasa kipo kwenye hatua mbalimbali kukamilika
Amesema sababu kubwa ya MSD kuja na Kampuni tanzu ni kwa lengo la kuondoa urasimu kwenye upatikanaji na usambazaji wa Dawa na kuongeza tija wanayoitarajia.
Amesema kuwa endapo kutakuwa na uhitaji Kampuni itakuwa inazitazama fursa na hivyo kuingia ubia na Wadau wengine utakaosaidia kuongeza uzalishaji.
“Ukishaongeza uwekezaji unaongeza wigo wa uzalishaji na hivyo kuruhusu Bohari ya Dawa ijikite katika Masuala ya ununuzi na utunzaji wa bidhaa za Afya”amesema Ibrahim
Aidha amesema kuwa wanatengeneza Mfumo imara ili kampuni hiyo iweze kujitegemea isiingiliwe kimaamuzi na hivyo kufika kule tinakotarajia.
Hata hivyo MSD Imeeleza kuwa itaendelea kusimamia uzalishaji ununuzi,utunzaj na usambazaji wa bidhaa za Afya kwenda kwenye Hospitali, Vituo vya kutolea huduma za Afya na Zahanati.