Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Bw. Mavere Tukai akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu utendaji wa bohari hiyo katika kazi hicho cha na Bohari ya Dawa.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daud Msasi akifungua kikao kazi cha Wahariri wa vyombo vya habari na Bohari ya Dawa kinachofanyika kwenye ukumbi wa Uchaguzi House Jijini Dodoma lengo la kikao kazi hicho likiwa ni kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu shughuli za Bohari ya Dawa nchini na majukumu yake kwa ujumla.
………………………………….
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
BOHARI ya Dawa (MSD) inatarajia kujenga maghala matano kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kagera, Dodoma na Mtwara ili kuboresha huduma za utendaji wa kazi zao.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika semina iliyoandaliwa na MSD ambayo inafanyika mkoani Dodoma.
“Maghala haya yatasaidia kuboresha huduma zetu za kusambaza dawa na vifaa tiba kwa wananchi hasa katika mikoa ambayo ina watu wengi kama Mwanza, Dar es Salam na Kagera” alisema Tukai.
Tukai alitaja mikoa ambayo yatajengwa maghala hao kuwa ni Kagera, Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam na Mtwara.
Akizungumzia maboresho ya utendaji kazi wa MSD alisema wameanzisha mfumo wa kufanya kazi kwa njia ya mtandao na kuachana na ule wa kutumia makaratasi jambo ambalo litaongeza ufanisi wa kazi na kila jambo kuwa wazi.
“Tumeanza kufanya majaribio kwa kufanya kazi kwa njia ya mtandao tena kwa uwazi ambapo kila mtumishi wetu atakachokuwa akikifanya kitaonekana jambo ambalo litasaidia kuondoa changamoto na urasimu kazini” alisema Tukai.
Alisema hakuna sababu ya kuficha taarifa za umma kwani kila mtu anatakiwa kuziona na kupitia mfumo huo wa njia ya mtandao wataweza kuwabaini wafanyakazi wao pale watakapokuwa wakifanya kazi chini ya kiwango.
Aidha Tukai alisema MSD inatarajia kufungua Kampuni Tanzu ambayo itasimamia viwanda vya uzalishaji ambavyo vitaendeshwa na MSD.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wakati akifungua semina hiyo alisema Serikali imetoa fedha Sh.Bilioni 200 kwa ajili ya kununua dawa na vifaa tiba lakini fedha ambazo zimepokelewa na MSD ni Sh. Bilioni 145.9.
Aidha Msasi aliwataka wahariri wa vyombo vya habari kuwasiliana na wahusika kabla ya kutoa habari ambazo zinaweza kuleta taharuki kwa wananchi hasa zile zinazohusisha afya za watu.
Msasi alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai kwa kuboresha mambo kadhaa ya MSD kwa muda wa miaka miwili ya ufanyaji kazi wake tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo Bw. Gerson Msigwa akitoa ujumbe wake wa wahariri wakati wa kikao kazi cha Wahariri wa vyombo vya habari na Bohari ya Dawa kinachofanyika kwenye ukumbi wa Uchaguzi House Jijini Dodoma lengo la kikao kazi hicho likiwa ni kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu shughuli za Bohari ya Dawa nchini na majukumu yake kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Bw. Mavere Tukai akiwasilisha mada kuhusu utendaji wa bohari hiyo katika kazi cha Wahariri wa vyombo vya habari na Bohari ya Dawa kinachofanyika kwenye ukumbi wa Uchaguzi House Jijini Dodoma lengo la kikao kazi hicho likiwa ni kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu shughuli za Bohari ya Dawa nchini na majukumu yake kwa ujumla.
Hipoliti Lello Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF akimwakilisha mkurugenzi wa mfuko huo katika kutoa salamu kwa washiriki wa kikao kazi hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bohari ya Dawa Etty Kusiluka akitoa utaratibu wa uendeshaji na uwasilishaji wa mada katika kiko hicho.
Picha mbalimbali zikionesha wahariri na waandishi wakiwakatika kikao kazi hicho.
Mwenyekiti wa Jukwaala Wahariri Tanzania TEF Bw. Deodatus Balile akifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitwasilisha na wawasilishaji.