Mkurugenzi wa Msama Promotion BwAlex Msama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka linalotarajiwakufanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es SalaamAplili 9,2023.
Mkurugenzi wa Msama Promotion BwAlex Msama akizizitia jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka linalotarajiwakufanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es SalaamAplili 9,2023 , kushoto ni mratibu wa Tamasha hilo Bw. Emmanuel Mabisa.
……………………………………………..
Rais wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania Samia Hassan Suluhu amethibitisha kuwepo kwenye tamasha la pasaka huku akimwagiza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh.Nape Nnauye kwa niaba yake Aprili 9, mwaka huu viwanja vya leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion BwAlex Msama , ambaye pia ndiye mwandaaji wa tamsha hilo amesema maandalizi yako vizuri kabisa na kila kitu kinakwenda sawa.
“Maandalizi yamekamilika asilimia mia moja na sasa kilichobaki ni watu kujiandaa na tamasha hilo wajitokeze kwa wingi.”
Pia ameongeza kuwa waimbaji wote wapo tayari wameshaanza kuingia nchini na mazoezi ya kutosha yaandelea kwa ajili ya tamasha hilo.
“ wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa ya jirani ya Pwani na Morogoro wakae ya wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” amesema
Msama ametaja wasanii ambao watatumbuiza kwenye tamasha hilo kutoka nje ni Masi Masilia kutoka Congo Faustine Munishi kutoka Kenya, Tumaini Akilimali kutoka Kenya, Joshua Ngoma kutoka Rwanda na Nicole Ngabo kutoka Congo
Aidha, kwa upande wa wasanii wa injili kutoka hapa nchini watakaopamba tamasha hilo ni John Lissu, Upendo Nkone, Mashamsham Band na Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.
“Msisahau kuwa kutakuwa na michezo ya kutosha kwa watoto wazazi msiwaache mtakuwa mnaburudika huku watoto wakiwa wanacheza vyakula vya kutosha vitapatikana kwa bei nafuu kutok katika mgahaw wa Food Point.” amesema Msama.