Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa (katikati) waliokaa na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wa kwanza kulia waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa Manispaa ya Morogoro baada ya benki hiyo kutoa viti 100 na meza 100 na vifaa vya ujenzi wakati wa ugawaji wa vifaa vya elimu kwa ambapo taasisi hizo zimeokea msaada msaada wa vifaa vya sekta ya elimu vyenye jumla ya sh12.5milioni.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa wa kwanza kushoto na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wa kwanza kulia wakikabidhi sehemu ya vifaa vya ujenzi kwa viongozi wa shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere wakati wa hafla ya kupokea msaada iliyofanyika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Manispaa ya Morogoro ambapo taasisi hizo zimepokea msaada ya jumla ya sh12.5milioni.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Rebeca Nsemwa kushoto akipokea moja ya viti 100 na meza 100 kutoka kwa Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi wakati wa ugawaji wa vifaa vya elimu kwa shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa Manispaa ya Morogoro ambapo taasisi hizo zimeokea msaada msaada wa vifaa vya sekta ya elimu vyenye jumla ya sh12.5milioni.
………………………….
Morogoro.
Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya msingi Sinyaulime na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Bigwa (FDC) ikikabidhiwa meza na viti vikiwa na vyenye thamani ya sh12.5 milioni wakati wa hafla iliyofanyika Bigwa, ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha sehemu ya faida kwa jamii ikiwemo sekta ya elimu hapa nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo mjini hapa, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi amesema benki hiyo imekabidhi meza 100 na viti 100 kwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Manispaa ya Morogoro wakati shule ya msingi Sinyaulime iliyopo kata ya Ngerengere ikikabidhiwa vifaa vya ujenzi.
Mlozi amesema benki ya imekuwa na utamaduni wa kutoa misaada kunatokana na faida wanayopata kila Mwaka na asilimia moja ya faida hiyo kuipeleka kwenye huduma za kijamii.
Mlozi amesema kuwa benki ya NMB imekuwa ikisapoti serikali katika kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo sekta ya elimu, afya kwa kutoa vifaa na majanga yanapojitokeza ikiwemo kimbunga, matetemeko ya ardhi na mafuriko yanayowakumba wananchi.
Mkuu wa chuo hicho, Dismas Mguba alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto za uhaba wa vitanda kwa wanafunzi wa bweni na kuomba wadau wengine kuiga mfano wa benki ya NMB kusapoti kusaidia vitanda.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Sinyaulime, Rahabu Kisunga amtoa shukrani kwa uongozi wa NMB kutokana na msaada wa vifaa vya ujenzi, bati, kenchi na misumari kwa ajili ya kupaua ambavyo vitasaidia kumalizia ujenzi wa chumba kimoja cha darasa la pili na la tatu ambavyo wayoyo husongamana kwenye chumba kimoja wakati wa masomo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Rebeka Nsemwa ametoa wito kwa jamii kutunza vifaa na misaada iliyotolewa na na benki hoyo ili viweze kudumu kwa kipindi kirefu kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vya baadae.