Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya na mimea Tanzania (TPHPA) ,Prof. Joseph Ndunguru akizungumzia mafanikio ya miaka miwili ya Rais Samia ofisini kwake.
……….,………
Julieth Laizer,Arusha.
Arusha.Mamlaka ya Afya na mimea Tanzania (TPHPA) katika kuadhimisha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan ,serikali imeweza kuboresha maabara ambazo zinaangalia ubora wa viatilifu ambavyo vinatumika hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA ,Prof. Joseph Ndunguru wakati akizungumzia mafanikio hayo ofisini kwake.
Amesema kuwa,maabara hiyo imekuwa ikitumika kupima ubora wa viatilifu na matokeo yake yamekuwa yakitambulika nchi nzima na kuleta mafanikio makubwa sana .
Aidha amesema kuwa, kupitia maabara hiyo wameweza kutoa mafunzo kwa wakulima na wadau mbalimbali juu ya matumizi ya maabara hiyo na kuweza kupunguza changamoto mbalimbali kwa wakulima kwa ujumla.
Ameongeza kuwa, wameweza kutoa mafunzo namna ya kudhibiti visumbufu vya mimea na kudhibiti milipuko ya visumbufu vya mazao ambapo hadi kufikia febuari mwaka huu wameweza kudhibiti kwelea kwelea milioni 227 kwa hekta elfu moja .
Ameongeza kuwa , aina 11 ya wadudu rafiki wameweza kusajiliwa na kudhibiti visumbufu vya mimea ambapo mamlaka hiyo imekuwa ikifanya kaguzi mara kwa mara katika maduka ili kudhibiti kuwepo kwa viatilifu bandia ambapo hadi febuari mwaka huu walifanikiwa kukagua mikoa 13 .
Ndunguru amesema kuwa,serikali pia katika kuboresha mamlaka hiyo imenunua Ndege nyuki ambazo zinawezesha kufanya survey katika maeneo yenye viasharia ambapo mikakati hiyo inalenga kuboresha shughuli za kilimo kwani wakulima wataweza kulima kilimo chenye tija na kuweza kufanya biashara na kupata kipato na kuweza kupunguza kwa matokeo ya viatilifu feki.
Aidha akizungumzia mafanikio mengine amesema kuwa, katika mamlaka hiyo kuna benki ya mbegu ambayo inasaidia kuhifadhi aina za mbegu ambazo zimekuwa zikileta manufaa makubwa sana kwa wakulima .
“Katika mamlaka yetu tumekuwa tukiwatumia wataalamu wetu kutoa mafunzo kwa wakulima ambapo wakulima wameweza kunufaika kwa kiwango kikubwa sana na kuweza kukuza kilimo chao na kuondokana na kilimo cha mazoea na tumeona mafanikio makubwa sana kwa wakulima hao.”amesema Dokta Ndunguru.
Mwisho.