Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akionyesha malighafi za mawe wanazotumia kuzalisha Gundi Yapfix mbayo ni maalum kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Alex Kaaya, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar ers Salaam kuhusu Gundi maalum ya Yapfix inayotumika kubandikia vigae (tiles) ukutani na sakafuni kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Necmetin Keles na Fundi Shabani Athuman (kushoto).
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing, Necmetin Keles, akionyesha jinsi bidhaa yao aina ya Yapfix inavyotumika kuzuia unyevu ukutani kwenye nyumba ambayo ina uwezo mkubwa wa kuizuia unyevunyevu unaosababishwa na maji ukutani, jijini Dar es Salaam.
………………………………
Kiwanda cha Bosphorus Manufacturing kinachojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za kujengea kimewashauri watanzania kutumia bidhaa za kampuni hiyo ili kuzifanya nyumba zao zidumu muda mrefu zaidi.
Hayo yamesemwa na meneja masoko wa kiwanda hicho Alex Kaaya mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza juu ya bidhaa ya kampuni hiyo iitwayo Yapfix wall putty inayotumiwa kwenye kuta za nyumba wakati wa kupaka rangi.
Amesema kupitia Yapfix wallputty sasa watanzania hawatakuwa na hofu ya kuhofia kuta za nyumba zao kupata fangus kwani imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ambao utaifanya kuta za nyumba kutopata magonjwa wala bakteria.
Amesema kwa kipindi hiki cha mvua katika maeneo mbalimbali nchini ni muhimu kwa watanzania kutumia bidhaa ya Antifangus Wallputty ambayo haiingizi maji kwenye ukuta na kuifanya rangi kubanduka hivyo nyumba itakaa muda mrefu sana baada ya kupakwa bidhaa hiyo.
Aidha ameongeza kuwa kwa kutambua pia umuhimu wa kuweka vigae (tiles) katika nyumba wamekuja na gundi maalum ambayo hutumika kuwekea tiles katika nyumba bila kuichanganya na mchanga wala saruji na badala yake hutumia maji pekee katika uchanganyaji wake.
Amesema imefika wakati sasa kwa watanzania kufanya ulinganifu wa bidhaa za Wallputt kutoka kampuni hiyo na kampuni nyingine ili kugundua ubora wa bidhaa za kiwanda hicho ambacho kimewekeza zaidi ya bilioni 2 hapa nchini
“Napenda kuwaambia mafundi kuwa wakati wa kuchanganya saruji na mchanga katika kuweka tiles majumbani imepitwa na wakati kwani kwa sasa sisi kama kiwanda cha Bosphorus tumekuja na gundi maalum ya kuwekea tiles ambayo hutumia maji pekee katika uwekaji wake”alisisitiza Bw Kaaya.
Hata hivyo ameongeza kuwa kiwanda hicho hutumia teknologia ya kituruki katika uandaaji wa bidhaa zake jambo ambalo limeongeza ubora wa bidhaa
Kuhusu ajira katika kiwanda hicho amesema wameajiri zaidi ya watu 35 ambao hufanya shughuli za uzalishaji kiwandani hapo ambapo asilimia kubwa ya uzalishaji wa bidhaa hutegemea teknolojia huku malighafi za kutengeneza bidhaa za kiwanda hicho ikiwemo mawe na mchanga zikinunuliwa kutoka kwa wafanyabishara hapa hapa nchini.
Kwa upande wake Bw Ramadhan Hassan ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa za ujenzi katika eneo la Tabata amewaambia waandishi wa habari kuwa tangu aanze kuuza bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho zaidi ya miaka saba iliyopita mpaka leo amekuwa akipata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wake wakieleza ubora wa bidhaa za kampuni hiyo.