Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio akizungumza wakati wa kikao na Wafanyabiashara na waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi jijini Dar es Salaam Kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu FCC, Nsajigwa Wilfred,Mkurugenzi wa Idara ya udhibiti wa bidhaa bandia, Khadija Ngasongwa na Mkuu wa Idara ya udhibiti wa bidhaa bandia, Salvertory Chuwa (kulia)
Mkurugenzi wa Idara ya udhibiti wa bidhaa bandia, Khadija Ngasongwa (katikati), akizungumza wakati wa kikao na Wafanyabiashara na waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu FCC, Nsajigwa Wilfred. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya FCC leo.
…………………………
Wafanyabiashara na waagizaji bidhaa nchini wametakiwa kufuata sheria za uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kuacha kukwepa kodi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio akizungumza wakati wa kikao na Wafanyabiashara na waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi jijini Dar es Salaam
Erio amesema, kuna changamoto kubwa ipo katika uagizizaji wa bidhaa nchini kutoka kwa wafanyabishara na mawakala ambao wengi wamekuwa wanashindwa kufuata sheria za uingizaji wa bidhaa hizo kama inavyotakiwa na serikali.
“Lengo la mkutano huu ni kuzungumza na wafanyabishara na wale waagizaji wa bidhaa kitoka nje ya nchi ambapo kuna changamoto kubwa katika uingizaji wa bidhaa hizo na wengi wamekuwa wanainyima serikali kodi kwa kusingizia bidhaa hizo kwa matumizi binafsi ikiwa sio kweli,”amesema
Erio ameeleza kuwa, wafanyabiashara wanatakiwa kujua bidhaa wanazoagiza zinatakiwa kujulikana inatoka nchini gani, iwe na anwani ya mzalishaji na iwekwe alama ya trademark ili ijulikane kama bidhaa hiyo imekopiwa au ni origino
Akizungumzia uingizwaji wa biashara, Erio amewataka wafanyabiashara hao na waingizaji wa bidhaa kufuat sheria zilizowekwa na kulipia kodi ili serikali iweze kufanya maendeleo.
“Mnavyokua wadanganyifu kwa kuingiza bidhaa ambazo mnasema mnaenda kwenye miradi ila kwa uhalisia mnaenda kuuza bidhaa hizo jambo ambalo sio sahihi kwahiyo sisi kama FCC tunawaagiza waagizaji wa bidhaa wawe wafanyabiashara au mawakala kuacha kufanya udanganyifu,”amesema
Naye Mkurugenzi wa Idara ya udhibiti wa bidhaa bandia, Khadija Ngasongwa amewataka wafanyabiashara kuagiZa vitu au bidhaa zinazo na uhalisia na zenye ubora ili kuacha kukamatwa kwa bidhaa zao na kuacha kutoa malalamiko kwa serikali.
Ameongeza kuwa FCC inatakiwa kujiridhisha na bidhaa zinazoagizwa ili kujua kama ni za matumizi ya kawaida au biashara na kusisitiza wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa kuendelea kufuata sheria kwani taaisisi yao haitaacha kukamat bidhaa zao pindi wanapoona hazijakidhi vigezo