Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene kushoto akimpongeza Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) kilichopo chini ya mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) akiwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Balozi wa Tanzania nchini Sudan kusini Balozi John Simbachawene akiwa Katika picha ya pamoja na Bw. Benson Meikoki Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda cha madawa cha Kairuki (KPIL) mara baada ya kuwasilisha mada Katika kongamano la msafara wa kibiashara wa Tanzania uliotembelea nchini Sudan Kusini Katika jiji la Juba ili kuangalia fursa mbalimbali kibiashara na uwekezaji Katika sekta ya Kilimo afya na Elimu.
Picha ya pamoja
Picha mbalimbali zikionesha Washiriki wa kongamano Hilo waliokuwemo Katika msafara huo wa kibiashara ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE
…………………………
Meneja Mauzo na Masoko Kiwanda Cha Madawa Cha Kairuki Pharmaceutical industry LTD(KPIL) Bw. Benson Meikoki amesema wataendelea kushirikiana na nchi mbalimbali Afrika Kwa kuwapatia Maji tiba (Drips) na Dawa za maji wanazozitengeneza katika Kiwanda hicho Ili kuendelea kutanua wigo wa sekta ya Afya katika Mataifa hayo.
Meikoki ameeleza hayo jijini Dar es salaam wakati wa majumuisho ya safari yao, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu safari yao ya kibiashara ambayo wamefanya nchini Sudan Kusini ambayo iliandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Baishara Tanzania TANTRADE
Amesema Kiwanda hicho kilipata fursa ya kushiriki msafara wa kibiashara baina ya nchi ya Tanzania na Sudan Kusini ambapo walikuwa na wadau wa sekta ya Afya, Kilimo na Elimu na wajasiriamali Ili kujadili namna gani Tanzania itaweza kushirikiana na nchi ya Sudan Kusini katika sekta hizo.
Amesema Kiwanda Cha Madawa cha Kairuki(KPIL) ndio kilipewa dhamana ya kunadi sera zake kama mwakilishi wa Viwanda vya madawa Tanzania ambapo alielezea Masuala mbalimbali , awali alielezea Mtandao wa mashirika ya Kairuki (KHEN) ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Kairuki ambayo imekuwa ikiendelea kuwa Hospitali bora nchini toka mwaka 1987.
Aidha amesema katika Hospitali hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani pia wamefungua kituo cha Upandikizaji Mimba (Kairuki IVF) kilichopo Bunju mazizini Ili kuweza kurahisisha huduma hiyo kupitia Wataalamu waliobobea kama vile Dkt. Clementina Kairuki na hivyo kuepusha gharama za safari za kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hiyo.
“Kupitia Mkutano huu tuliweza kueleza kuwa kwa sasa Afrika haiwezekani kutokuwa na mtoto bali anapatikana KAIRUKI IVF alisema Meikoki, pamoja na mambo mengine alisema mtandao huo wa KHEN una chuo kikuu cha madaktari , na chuo cha manesi.
Meneja Huyo ameendelea kusema Kiwanda Cha Kairuki kimeweza kutengeneza na kuzalisha chupa Mill 60 Kwa Mwaka lakini pia kuajiri wafanyakazi zaidi ya 500.
Amesema miongoni mwa madawa mbalimbali ambayo yanazalishwa katika Kiwanda hicho ni pamoja Ringer Lactate,Mannitol, Paracetamol,Fluconazole,Ciprofloxacin,Sodium chloride 3% , DNS, NS, D5, D10, D50, na Nyingine nyingi.
Amesema pia wanafanya Biashara na wadau mbalimbali zikiwemo za ndani kama vile Msd Tanzania bara, CMS zanzibar visiwani, na mahospitali kama vile Muhimbili, Lugalo,Rabininsia, TMJ na nyingine nyingi na biashara za Nje kama vile Malawi,Zambia,Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Yemen,pamoja na nchi nyingine ambazo wapo kwenye hatua za mwisho za makubaliano.
Aidha ameeleza lengo na madhumuni ya Kiwanda hicho ni kuweza kuzihudumia nchi za SADC kwani katika safari hiyo wamefanya mazungumzo na Sudan kusini Ili kuangalia uwezekanao wa kufanya biashara na kupeleka madawa katika nchi hiyo.