Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari wakatialipokuwa akitoa taarifa kuhusu ziara ya Makamu wa Rais waMarekani Kamala Harris itakayoanza Machi 29 mpaka Machi 31, 2023.
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Stergomena Tax akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa taarifa kuhusu ziara ya Makamu wa Rais waMarekani Kamala Harris itakayoanza Machi 29 mpaka Machi 31, 2023. kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi Dkt. Elsie Kanza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi Mindi Kasiga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje wakati akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribishwa ili kuzungumza na waandishi wa habari wakatialipokuwa akitoa taarifa kuhusu ziara ya Makamu wa Rais waMarekani Kamala Harris itakayoanza Machi 29 mpaka Machi 31, 2023.
*Wananchi waombwa kumpokea Kamala Harris, Serikali yatarajia neema
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA hasa wananchi wa jiji la Dar es Salaam, wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ambaye anatarajiwa kutembelea Tanzania kuanzia tarehe 29 hadi 31 Machi 2023, kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Stergomena Tax leo leo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo ameweka bayana kuwa ujio wa Kamala utakuwa neema kwa Tanzania kiuchumi, kijamii na diplomasia.
Amesema Kamala atapokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt Philip Mpango Machi 29, 2023 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Machi 30 atafanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dkt Tax amesema Makamu wa Rais Kamala na ujumbe wake watatembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kukutana na vijana wajasiriamali wa Tanzania.
Waziri Tax amesema baada ya shughuli hizo za kikazi, Kamala atashiriki futari na iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Samia siklu y.a Alhamisi Machi 30, 2023.
“Pamoja na mambo mengine, ziara hii ya Mheshimiwa Kamala nchini Tanzania inalenga kuongeza nguvu katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania hususan baada ya kufanyika kwa mkutano kati ya Marekani na nchi za Afrika maarufu kama US – Africa Summit mwezi Desemba 2022, ambapo Rais Samia alihudhuria.
Ziara hii ni ya kihistoria ambapo Makamu wa Rais wa Marekani ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo, anafanya ziara ya kikazi Tanzania na kukutana na Rais Samia, ambaye pia ni Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ziara hii inafanyika takriban miezi 11 tangu viongozi hawa wawili wanawake walipokutana Ikulu ya Marekani na kubadilishana mawazo juu ya majukumu yao katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani uliodumu kwa miongo mingi tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa,” amesema.
Aidha, amesema ziara ya Kamala nchini Tanzania inalenga katika kuunganisha nguvu za ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi Tanzania na Marekani katika sekta za afya, kilimo, utalii, uchukuzi, uchumi wa buluu, mawasiliano, uchumi wa kidijitali, uungaji mkono hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uhimilivu wake na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kupitia ubunifu, ujasiriamali na uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Amesema Marekani imesajili miradi 266 yenye thamani ya dola za Marekani zaidi 4,000, ambayo imetoa ajira 54,584, hivyo matumaini yao ni kuona baada ya ziara hiyo wawekezaji wataongezeka.
Tax amesema kwa miaka ya hivi karibuni sekta ya utalii imepokea watalii wengi kutoka Marekani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2022 wamepokea watalii 100,600 kutoka watalii 66,394 mwaka 2015.
Makamu wa Rais Kamala ataambatana na mumewe ambaye atafanya mikutano na wadau wa michezo na utunzaji wa habari kupitia program ya Tuheshimu Bahari.
Waziri Tax amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu ambazo Mheshimiwa Kamala na ujumbe wake watazitembelea ndani ya bara la Afrika ambapo ameanza ziara yake tarehe 25 hadi 28 Machi nchini Ghana na nchi nyingine ni Zambia.