SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewataka maafisa habari kutoa taarifa sahihi kwa wakati ili wananchi waweze kupata habari isiyokuwa na ukakasi wowote ule.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao kazi Cha maafisa uhusiano na Mwasailiano Serikalini kinachofanyika kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam,Dkt Tulia alisema kuwa maafisa habari wanatakiwa kutengeneza mahusiano mazuri na waandishi wa habari na wadau wa habari ili kuondoa taarifa za upotoshaji kwa jamii.
Dkt Tulia alisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wanakosa habari kutokana na maafisa habari kushindwa kutoa ushirikiano na hao waandishi.
“Maafisa wa habari wa bunge wanatakiwa kujenga mahusiano na waandishi pamoja na wabunge ili kuondoa taarifa za upotoshaji kwa kuandika taarifa kamili kwenye tovuti husika ili kusiwe na upotoshaji”alisema Dkt Tulia
Aidha Dkt Tulia aliwataka maafisa habari kusoma na kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwa serikali ya awamu ya sita inatokana na chama hicho.