……………,………
Serikali imesema itaendelea kushughulikia mapungufu na mahitaji yanayohusu utoaji wa Huduma za Hali ya Hewa nchini kwa nia ya kuboresha huduma za tahadhari zinazoendana na kasi na kukabiliana na maendeleo ya kimataifa ya sayansi na teknolojia,
Kauli hiyo imetolewa jijiji Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kilele cha Maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani ambayo imekwenda na kauli mbiu isemayo “Mustakabali wa Hali ya Hewa, Tabianchi na Maji kwa Vizazi Vyote”
Amesema mpango huo umelenga kuhakikisha kila mtu alindwe kwa kupata taarifa za tahadhari ndani ya miaka mitano kuanzia mwaka 2022.
Aidha amesema kuwa utoaji wa huduma bora za hali ya hewa na maji umekuwa kipaumbele cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu zote hivyo watahalikisha wanaendelea kuijengea Taasisi hiyo Mazingira mazuri.
“Huma hizi zina umuhimu mkubwa na huongeza tija katika maendeleo ya sekta zote za kijamii na kiuchumi lakini pia Utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini Tanzania ulianza kabla ya uhuru ambapo upimaji wa hali ya hewa ulianza mwishoni mwa miaka ya 1800. Mfano kituo cha kwanza cha hali ya hewa kilianzishwa mwaka 1892 katika mji wa Bagamoyo. Kuanzia mwaka 1929, huduma za hali ya hewa zilitolewa na iliyokuwa Taasisi ya Hali ya Hewa chini ya Serikali ya Kikoloni ya Uingereza katika nchi za Afrika Mashariki “The British East Africa Meteorological Services (BEAMS)”. Makao Makuu ya taasisi hiyo yalikuwa Tabora.”alisema Naibu Waziri Mwakibete
Aidha Naibu Waziri Mwakibete amesema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na taarifa za uhakika za hali ya hewa, Serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini ikiwemo Miongoni mwa maeneo ya uwekezaji mkubwa ni ununuzi wa miundombinu ya kisasa ya uchunguzi wa hali ya hewa ikiwa ni pamoja na RADA za hali ya hewa.
Pia amesema kuwa eneo jingine ni kujenga uwezo wa rasilimali watu kwa uanzishwaji wa Shahada ya Kwanza ya Hali ya Hewa na Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo Endelevu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na upanuzi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa kilichopo Mkoani Kigoma.