Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti Ndg Marry Chatanda (Kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti Ndg. Zainab Shomari (Kulia) iliyotolewa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) Ndg. Marry Chatanda akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Siku Mbili kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma. (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)
Meza kuu ikiimba Wimbo mara baada ya Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana alipowasili kufungua Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komred Abdulrahman Kinana Akipokea tuzo ya pongezi kwa Kuchaguliwa kuendelea kuwa Makamu Mwenyekiti wa (CCM) Tanzania Bara kwa Mwenyekiti Ndg Marry Chatanda (Kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti Ndg. Zainab Shomari (Kulia) iliyotolewa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT) kwa Wajumbe wa Baraza kuu ,Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji CCM)
………………………………
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amewataka viongozi wa CCM wayaeleze kwa wananchi mambo mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kinana aliyasema hayo jijini hapa jana, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya.
“Katika maeneo yenu hakikisheni mnakisemea Chama na mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, wala msione haya kusema ili wananchi wajue na hata katika chaguzi zijazo tusipate shida.
Alisisitiza kuwa: “Chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka miwili kila kata kuna alama ya maendeleo kuanzia shule, zahanati, barabara na maendeleo ya watu, tuna kila sababu ya kujisifia na kuusifia uongozi wa mwenyekiti wa chama hiki.”
Vilevile, Kinana aliwataka viongozi wa UWT kubeba ajenda za wanawake kitaifa bila kuogopa jambo lolote.
Akizungumzia kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Kinana aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufia lengo la kujenga jamii yenye usawa.
Alisema mwakani kuna uchaguzi wa viongozi wa serikai za mitaa, hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuchukua fomu kuomba nafasi mbalimbali za uongozi na CCM itawapa ushirikiano wa kutosha.
“Kuelekea uchaguzi ujao jiandaeni na kuwahimiza wanawake kuwania nafasi zote za uongozi na ninawahakikishia kuwa, CCM itawaunga mkono kwa hali na mali ili kuwa na wanawake wengi waliochaguliwa katika majimbo,”alisema.