Mkurugenzi wa Huduma za Tahimini WCF, Dkt Abdulsalaam Omary akitoa mada katika kikao kazi kati ya wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF na Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi WCF kinachofanyika mjini Bagamoyo katika hoteli Stella Maris mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Huduma za Tahimini WCF, Dkt Abdulsalaam Omary na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mdumawa kimsikiliza Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF alipokuwa akizunguma jambo katika kikao hico
………………………………………
Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi-WCF, umesema umekuja na mpango wa kuzuia upigaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya wafanyakazi kwa kutengeneza ajali au ugonjwa ili kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo pale mfanyakazi anapoumia sehemu ya kazi.
Mkurugenzi wa huduma za tathimini WCF, Dkt Abdulsalaam Omary amesema hayo katika kikao kazi kati ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi na Jukwaa la wahariri kinachofanyika mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Katika kikao kazi hicho, Dkt Omary amesisitiza kuwa zamani baadhi ya wafanyakazi walikuwa wanasababisha mfuko huo kupata hasara kwa kuingiza madai ambayo hayana ukweli kwa kutengeneza ajali ili kujipatia fedha zinazotokana na mafao yasiyowahusu kupitia mfuko huo.
Lakini sasa baada ya kuja na mfumo maalumu wa kufuatilia au kufanya tahimini wamekuwa wakibaini uongo unaofanya na wafanyakazi ili kujipatia tu fedha za madai.
Ikumbukwe kuwa sio kila ajali inayoipata mfanyakazi akiwa sehemu ya kazi atalipwa fidia, ila atapata tu fidia baada ya tathimini ya kina kutoka kwa wataalamu wa WCF ndio atapata mafao hayo.
Akitolea mfano Dkt. Omary amesema WCF wamewahi kupata kesi ya mgonjwa kudai kuwa ameumia sehemu ya kazi na kuumia uti wa mgongo ambao ulisababisha kushindwa kupoteza nguvu za kiume, lakini uchunguzi ulipofanyika ilibainika madai hayo hayakuwa na ukweli, lengo lilikuwa ni kujipatia mafao ambayo hayamuhusu.
Baadhi ya wahariri waiwa katika kikao hicho.
Laura Kunenge Mkuu wa Uhusiano Kwa Umma WCF akirekodi jambo katika kikao hicho.
Laura Kunenge Mkuu wa Uhusiano Kwa Umma WCF akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa mitandao ya Fullshangwe Bw. John Bukuku wakati wa kikao hicho.
Picha ya pamoja.