Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akifungua Kikao kazi cha wahariri kati ya Taasisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF inayofanyika kwenye hoteli ya Stella Maris Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 20, 2023 kulia ni Abdullsallaam Omar Mkurugenzi wa Tathmini WCF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma na Dkt.Abdullsallaam Omar Mkurugenzi wa Tathmini WCF wakimsikiliza Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF wakati akizungumza kwenye Kikao kazi cha wahariri kati ya Taasisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF inayofanyika kwenye hoteli ya Stella Maris Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 20, 2023.
Abraham Siyovelwa Mkuu wa Huduma za Sheria WCF akitoamada katika kikao kazi hicho kinayofanyika kwenye hoteli ya Stella Maris mjini Bagamoyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma na Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF wakifuatilia mada katika semina kikao kazi hicho.
Baadi ya wahariri kutoka TEF wakiwakatika Kikao kazi hicho.
Bw. Anselim Peter Mkurugenzi wa Ueneshaji WCF akifafanua jambo kuhusu shughuli na jinsi Mfuko wa WCF unavyotambuliwa Afrika na Dunia kutokana na Utendaji wake.
Dkt.Abdullsallaam Omar Mkurugenzi wa Tathmini WCF akitoa mada katika semina hiyo.
Serikali ya awamu ya sita ambayo inaogozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani awamu hii imehakikisha mfuko huo unaweza kujiendesha kwa uwiano kati ya serikali na sekta binafsi kwa kupunguza riba na kubaki kulipa deni msingi lisilokuwa na riba.
Haya yamefaywa na awamu ya sita ili kuufanya Mfuko wa Fidia kwa Wafayakazi WCF kutokuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi kwani kabla ya mwaka 2021/2022 wafanyakazi wa sekta binafsi walitakiwa kuchangia asilimia 1 ya mshahara kwa mfanyakazi ambapo serikali ilishusha mpaka kufikia asilimia 06 na mwaka huu wa fedha imepunguza mpaka asilimia 0.5 jambo ambalo limeleta unafuu sana kwa sekta binafsi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Mfuko wa Fidia kwa Wafayakazi WCF wakati akifungua Kikao kazi cha wahariri wa vyombo kutoka Jukwaa la wahariri TEF leo katika Hotel ya Stella Maris Bagamoyo, mkoani Pwani kinayofanyika kwa lengo la kufafanua mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya mfuko huo wa fidia kwa wafanyakazi katika taifa.
Ameongeza kuwa Serikali pia imepunguza riba ya wale waliokuwa wakichelewesha michango ambapo ukichelewesha kujisajili na kuwasilisha michango ulitakiwa kulipa riba asilimia 10 kwa mwezi na kwa mwaka ilikuwa zaidi ya asilimia 120 na sasa imepunguza mpaka asilimia 2 tu jambo ambalo lilikuwa linawaumiza sana na sasa wamepata unafuu mkubwa.
Amesema mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kama taasisi ya hifadhi ya jamii chini ya ofisi ya Waziri mkuu ikiwa na majukumu ya kuwafidia wafanyakazi wanaopata magonjwa na ajali au kufariki watakapokuwa katika majukumu yao ya kazi katika taasisi na mashirika mbalimbali imefanya kazi kubwa na kuchangia maendeleo ya nchi hasa katika uwekezaji kutokana na huduma ambazo mfuko huo umeendelea kutoa kwa wafanyakazi.
ametanabaisha kwamba mfuko wa WCF unategemea wadau mbalimbali kuuchangia wakiwemo wafanyabiashara na serikali, Lakini pia mfuko huo una wadau wa kati ambao wanauwezesha likiwepo Jukwaa na wahariri TEF.
“Jukwaa la wahariri ni wadau muhimu kwa WCF kwa sababu ushirikiano kati ya WCF na vyombo vya habari ni muhimu sana katika kutekeleza majukumu yake kama taasisi inayofanya kazi zake lakini pia kutangaza na kuelimisha umma kuhusu mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na taasisi hiyo,! Amesema Dkt. John Mduma
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania ndugu Deodatus Balile amesema wanaupongeza mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuweza pia kutatua changamoto zilizokuwa zinakuwa changamoto kwa wadau ndani ya mfuko huo.
“Sisi tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwani imeuwezesha mfuko huu kupunguza kiasi cha michango kutoka kwa sekta binafsi na sekta ya Umma na kupunguza mzigo mkubwa wa michango uliokuwa ukiwakabili waajiri,” Amesema Deodatus Balile.