…………………..
Dar es Salaam.
TAASISI ya Utafiti wa Kimataifa (NRF) kupitia vigoda vya Utafiti vya ufadhili wa mpango Oliver Tambo (O.R.) imetembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kujadili Maendeleo ya Vigoda vya Utafiti toka vianze kutekelezwa nchini Tanzania.
Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mitandao ya Maarifa na Mpango Mkakati toka Baraza la Utoaji wa Ruzuku za Sayansi (SGCI), Bi. Dorothy Ngila aliewasilisha muundo wa utendaji kazi wa Taasisi ya NRF kutoka Taifa la Afrika Kusini.
Akifungua Mkutano wa mapokezi ya ujumbe huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Bugwesa Katale leo tarehe 20 Machi, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa COSTECH.
Kwa upande wa COSTECH,Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) Dkt. Beatrice Lyimo aliwasilisha muundo wa utekelezaji wa kazi za COSTECH.