Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi katika Sherehe za kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda kabla ya kuhutubia Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
…………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wanawake kupaza sauti kwa pamoja na kukemea changamoto zinazowakabili wanawake wa Tanzania katika nyanja mbalimbali bila kujali itikadi zao.
Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akihutubia katika sherehe ya kilele cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru.
Aidha, Rais Samia ameahidi kuendelea kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili wanawake na kuwafanya kukosa huduma ikiwemo kujenga shule za wasichana za sayansi na vyuo vya ufundi ili kuwainua wanawake katika masuala ya kiteknolojia.
Kwa upande wa miundombinu, Rais Samia amesema Serikali imeweka bajeti ya kutosha kuiwezesha Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kuendeleza miundombinu ya barabara vijijini.
Vile vile, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kuimarisha Bandari za Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Mtwara na Kigoma ili kuimarisha biashara nchini na ndani ya bara la Afrika kwa ujumla.
Halikadhalika, Rais Samia amesema Serikali itasimamia Tanzania kuwa kinara wa uchumi kwa kumsimamia mwanamke kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazouzwa ndani na nje ya nchi kama ilivyopendekezwa na Jukwaa la Usawa wa Kijinsia.
Rais Samia pia ameeleza kuwa changamoto za mabadiliko ya tabia nchi zimesababisha kupanda kwa gharama za bidhaa hivyo, Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto hizo kuhakikisha Watanzania wanakuwa na ustawi mzuri wa maisha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda kabla ya kuhutubia Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia Wananchi wakati akiwasili katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Sherehe za Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) tarehe 19 Machi, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na Wananchi wa Mikoa mbalimbali wakiwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.
Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na Wananchi wa Mikoa mbalimbali wakiwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Kilele cha Miaka mawili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.