Mkurugenzi Mkuu Shirika la Mawasiliano Tanzania Mhandisi Peter Ulanga, amempongeza Mkurugenzi Mendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) pamoja na Watumishi wote wa Taasisi hiyo kwa kazi wanayoifanya katika kuwahudumia wagonjwa
Mkurugenzi huyo wa TTCL ametoa pongezi hizo kupitia kwa Afisa Uhusiano washirika hilo Bi Adeline Berchimance aliyeongozana na baadhi ya wafanyakazi Wanawake wenzake kwa niaba ya wafanyakazi wanawake wa shirika hilo nchi nzima wakati kwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo ya saratani ya Ocean Road ikiwa ni pamoja na kuwafariji.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Bi Adeline Berchimance amewshukuru wafanyakazi wa taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa juhudi mbalimbali wanazoziweka katika kuhakikisha wagonjwa wanaofikishwa katika hospitali hiyo wanapatiwa huduma stahiki huku wakitanguliza upendo na moyo wa kujitolea ili kuwarejeshea tabasam tena.
“Napenda kutumia fursa hii pia kuwapongeza wanawake wote katika Taasisi hii kwakutumia umama wao kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kama akina mama ndani ya taasisi na kama watumishi kitaaluma kutoa huduma kwa wahitaji hawa, ” amesema Bi Adeline Berchimance.
Ameoneza kuwa Machi 8 ya kila mwaka Wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania huungana na wanawake wenzao kusherehekea siku ya Wanawake Duniani ambapo pamoja na mambo mengine huyatumia maadhimisho haya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa nipamoja na kufanya usafi katika maeneo ya hospitali, kuchangia damu na kutoa zawadi ya vitu mbalimbali kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kibinadamu.
Hivyo uwepo wetu hapa ni sehemu ya namna yetu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani na lengo letu ni kuwapa pole wagonjwa na kuwapongeza wafanyakazi na watoa huduma kwa wagonjwa hawa upendo wanaouonesha katika nyakati zote wanapokuwa wanawahudumia.
“Tunatambua mnafanya kazi kubwa na pengine katika mazingira magumu lakini daima hamjawahi kuwaacha licha ya changamoto mnazokutana nazo. Kwetu sisi tunawaombea kwa Mungu asiwapungukie ili mzidi kuwa sehemu ya kuokoa maisha ya watu wake,” .AmesemaBi Adeline Berchimance
amesema kuwa zimeletwa zawadi ndogo za Pampasi Katoni 30, Sabuni ya unga viroba 7, mafuata ya kupaka katoni 4, Sabuni ya mche katoni 7 na pamoja na Dawa ya meno katoni 10 Tunalishukuru Menejimenti ya Shirika letu kwakuona umuhimu wa juhudi za wanawake wa TTCL na hivyo kutuunga mkono katika kufanikisha safari yetu ya kufika hapa kuwaona wagonjwa na kuwafariji.
Amesema zawadi hiyoo imetolewa na wanawake wa Shirika la Mawasiliano Tanzania kwa kuwezeshwa na Shirika letu kuja kuonesha upendo wetu kwa wagonjwa wetu hawa.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali, mwananchi mmojammoja, Taasisi na Kampuni mbalimbali ni kuendelea kujitoa kwa misaada ya hali na mali kwa Taasisi hiyo inayofanya kazi kubwa nchini kwani mahitaji ni mengi wanahitaji kushikwa mkono.
Aidha ametoa witi kwa wanafunzi walioko mashuleni hususani wa kike wajikite Zaidi katika kutengeneza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii ili kuwa sehemu ya wanawake wanaotoa huduma katika Taasisi hii na sehemu zingine kwa ustawi wa jamii nzima.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Bi Adeline Berchimance akikabidhi zawadi mbalibali kwa Mwanga Muhoki Muuguzi Msimamamizi wa wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI)wakati wanawake wafanyakai wa shirika hilo walipowatembelea wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo ili kuwajulia hali na kuwafariji.
Justine Chambo Afisa Maendeleo ya Jamii Taasisi ya Saratani ya ORCI akishukuru mara baada ya msaada huokutolewa kwa wagonjwa.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Bi Adeline Berchimance akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo.