Waziri wa Elimu, Sayansi na technolojia Profesa Adolf Mkenda akiongea na kamati ya kudumu ya ya Elimu, utamaduni na michezo mara baada ya kamati hiyo kutembelea Jengo la kituo cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa Muhas- Mloganzira.
………………………………..
kamati ya kudumu ya Bunge, Elimu, utamaduni na michezo leo imetembelea na kujionea ujenzi wa jengo la kituo cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya Damu kilichopo chini ya chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha muhimbili- Mloganzira ambapo kituo hicho kimejegwa ikiwa ni katika mikakati ya kukabiliana na magojwa yasiyoambukiza.
Kuanzishwa kwa kituo hicho itasaidia kutengeneza ajira, kukuza uchumi na kupunguza gharama za matibabu ya nje ya nchi kwa kuwa wagonjwa wengi watatibiwa hapa nchini vile vile wagonjwa kutoka nchi nyingine watatibiwa kwenye kituo hicho na itakuza uchumi na kutangaza utalii.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo Ubungo Mheshimiwa Kitila mkumbo amesema anakipongeza chuo cha Muhas kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa jengo hilo .
‘Tumetembelea kituo muhimu cha umahiri wa magonjwa ya moyo na mishipa ya Damu tumejionea shughuli zote za ufundishaji zimekamilika.
Amesema Kitila Mkumbo
Kuhusu ujenzi wa hospitali ya magojwa ya Moyo Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema watalifikisha jambo hilo sehemu husika ili lifanyiwe kazi kwa haraka kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Kwa upande wake waziri wa Elimu, Sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema serikali imefanya jambo kubwa katika kuweza ujenzi wa kituo hicho ambacho kitaleta manufaa na mapinduzi katika sekta nzima ya elimu ya kiudactari.
Kuhusu changamoto ambazo kamati hiyo imeeleza kukwamisha ndoto za baadhi ya wanafunzi haswa wa kike au kuwakatisha tamaa zikiwepo Rushwa za Ngono vyuoni Waziri amekemea vikali maprofesa na waalimu wanahusishwa na kashfa hizo huku akisema hatua kali zitachukuliwa, na ameendelea kuwahasa wanafunzi kutoa taarifa za unyanyasaji pindi wanapokutana nazo.
Aidha Waziri Mkenda amesema kuhusu suala la kutatishwa kukaa bwenini kwa wanafunzi chini ya Darasa la tano sio jambo la gafla kwani muongozo huo tangia tangia kipindi cha nyuma na maelekezo wamiliki wa shule wanayajua kwani kabla hawajafungua shule wanapewa miongozo ambayo moja ya sheria ni kutomuweka mtoto chini ya Darasa la tano bwenini.