Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Dialo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na watumishi wa TFRA Kanda ya Kaskazini katika ziara ya siku mbili kwenye kanda hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA, Anthony Dialo (kulia) akimsikiliza Kaimu Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Sheila Mrogoro akiwasilisha taarifa ya utendaji wa kanda yake kwa mwenyekiti aliyefanya ziara na kuzungumza na watumishi wa kanda hiyo.
Kaimu Meneja wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa TFRA, Belinda Kyesi akizungumza wakati wa kikao baina ya watumishi wa Mamlaka Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka Anthony Dialo tarehe 14 Machi, 2023 alipowatembelea ofisini kwao Jijini Arusha ili kubadilishana uzoefu na kufahamu ilipo ofisi hiyo kwa kanda ya Kaskazini
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Dialo (kulia) akisalimiana na Kaimu Meneja waKitengo cha Huduma za Sheria wa TFRA, Belinda Kyesi mara baada ya Mwenyekiti huyo kuwasili ilipo Ofisi ya Mamlaka kwa Kanda ya Kaskazini
Kaimu Meneja Uhamasishaji wa Uzalishaji wa mbolea na Utunzaji wa Mazingira wa TFRA Stephenson Ngoda akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya wafanyakazi wa TFRA kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TFRA, Anthony Dialo (kulia), Kaimu Meneja wa Huduma za Sheria wa TFRA, Belinda Kyesi (kushoto), Kaimu Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini Sheila Mrogoro (katikati) na Kaimu Meneja Uhamasishaji wa Uzalishaji wa mbolea na Utunzaji wa Mazingira wa TFRA Stephenson Ngoda wakielekea Ofisi ya TFRA kanda ya Kaskazini jijini Arusha.
……………………
Mwenyekiti Mteule wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony M. Diallo amewapongeza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya.
“Mnafanya kazi kubwa sana kwa idadi yenu huwezi kufikiri kuwa ndio mnaotekeleza majukumu haya mazito” Aliongeza Diallo.
Pongezi hizo amezitoa tarehe 14 Machi, 2023 alipoanza ziara yake ya siku mbili katika kanda hiyo ikiwa na lengo la kujifunza juu ya utendaji kazi wa viwanda vinavyozalisha mbolea pamoja na kuendelea kujifunza masuala mbalimbali yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo kwa vitendo.
Akizungumza na watumishi hao katika kikao kifupi kilichofanyika katika ofisi za kanda hiyo, Dkt. Diallo alieleza nia ya kuendelea kuboresha na kuimarisha mifumo inayosimamia Mamlaka ili kupunguza mianya ya upotevu wa fedha za Serikali.
Dkt. Diallo aliongeza kuwa, pamoja na kujifunza kutoka kwa wazalishaji wa mbolea yeye pia ni mbobevu katika eneo hilo na kueleza amejikita katika sekta ya viwanda kwa muda mrefu.
Akiwasilisha taarifa ya Kanda, Kaimu Meneja wa TFRA Sheila Mrogoro alisema, Kanda ya Kaskazini inasimamia mikoa 4 ikiwa ni (Mkoa wa) Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga.
Sheila alieleza kwa kifupi majukumu yaliyotekelezwa na Ofisi yake kwa Mwaka wa fedha 2022- 2023 kuwa ni pamoja na; ukaguzi wa wafanyabiashara na wazalishaji wa mbolea, ukaguzi wa nguzo (premises) za kuzalishia na kuhifadhia mbolea, kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wafanyabiashara wa mbolea ili kufikisha utaalamu huo kwa wateja wao(wakulima) na nyingine zilizomo ndani ya mamlaka yao.