Mratibu wa Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano Kituo cha TARI Mikocheni Vidah Mahava akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kuwaeleza kuhusu utafiti ambao unafanywa katikati kituo hicho.
Mtafiti katika Kituo cha TARI Mikocheni kwa upande wa maabara ya Tissue Culture Christina Kidulile akiwaonyesha wanahabari njia zinazotumika kuhifadhi Mbegu katika maabara hiyo.
Baadhi ya Mbegu ambazo zinafanyiwa utafiti katika Kituo cha TARI Mikocheni jijini Dar es salaam.
Wanahabari wakiendelea kupatiwa elimu ya namna mimea inavyozalishwa katika maabara ya maabara ya Tissue Culture iliyopo katika Kituo cha TARI Mikocheni
………………………..
NA MUSSA KHALID
Kituo cha Utafiti wa Kilimo Mikocheni jijini Dar es salaam kimepanga mikakati yao katika utafiti wanaoufanya kwa sasa ni kuwa na mbegu ambazo zinakinzana na magonjwa,ukame na zinazaa kwa wingi.
Pia imeelezwa mikakati hiyo ni pamoja na kushirikiana na Halmashauri mbalimbali nchini na wadau katika kugawa Mbegu ambazo zimefanyiwa utafiti kwenye mikoa ambayo inalima Nazi nchini ili waweze kustawisha vitalu vyao katika zao la minazi.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mratibu wa Uhaulishaji Teknolojia na Mahusiano Kituo cha TARI Mikocheni Vidah Mahava wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wametembelea Taasisi hiyo kujifunza kupitia Mafunzo ambayo wamepatiwa na Taasisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH ambapo amesema kumekuwa na changamoto kwa jamii kutokujua kuhusiana na kituo hicho lakini uzalishaji wa mbegu kwa njia ya Chupa.
‘Watu wengi wanakuwa na taarifa tofauti wengine wanafikiria kwamba tukienda Mikocheni kuwa ni GMO wanaiweka bioteknolojia na GMO kumbe yote hayo yanatokana na wananchi kutokuwa na taarifa kamili kuhusiana na kituo hiki na utafiti wetu unavyofanya kazi’amesema Vidah
Aidha amesema hicho ndicho kituo pekee kinachosimamia zao la minazi na malengo yao ni kuhakikisha kuwa linachangia pato la taifa na mazao ya mafuta.
Mratibu huyo amesema kwa sasa nazi wanazozigawa zinauwezo wa kuzaa nazi 35 mpaka 45 ambapo utafiti unataka kufika mpaka nazi 70 hivyo kuna mbegu ambazo wamekuwa wakizigawa kwa wadau wao.
Ameendelea kusema kuwa mikakati mikubwa ambayo wanaifanya ni kuhakikisha wanaweza kufanya kazi na wadau mbalimbali ili kufufua zao la minazi kwakutumia kanuni bora za kilimo.
Amesisitiza kuwa TARI inafanya utafiti wa mazao kwa kuvumbua mbegu kwa kutatua matatizo ya wakulima nchini ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mazao yao hususani wadudu.
Naye Mtafiti katika Kituo cha TARI Mikocheni kwa upande wa maabara ya Tissue Culture Christina Kidulile amesema katika maabara hiyo wanazalisha mimea ya aina ukiwemo Mkonge,viazi vitamu na wamekuwa wakitumia vifaa mbalimbali vinavyosaidia mimea kuota.
Kituo cha TARI Mikocheni ni moja ya vituo 17 vya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania –TARI hivyo imeelezwa dhamira yao kuhakikisha inaendelea kuwapatia elimu juu y utafiti wanaouchanya.