Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salam mkurugenzi wa huduma za uthibiti wa maabara ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali Daniel Ndiyo Amesema kwamba video inayosambaa mitandao ikieleza kuwepo na usafirishaji wa kemikali bila kufuata taratibu wala kuchukua tahadhari nchini Tanzania ipuuzwe kwani haina ukweli wowote huku akisema ofisi ya Mkemia mkuu ambayo ina mamlaka ya kusimamia sheria zote za usafirishaji wa kemikali hatarishi nchini wanafuata sheria zote za kimataifa na kitaifa.
Ameongeza kwamba kwamba mamlaka hiyo huwa inatoa elimu katika kuhifadhi na kusafirisha kemikali zenye sumu ambapo madereva wote wanaosafirisha kemikali hizo huwa wanapewa elimu na mafunzo ya kiusalama na namna ya kujikinga endapo ajali itatokea.
Aidha Daniel Ndiyo ameendelea kutoa ufafanuzi kwamba suala la kusafirisha kemikali yenye sumu lazima kuwe na msafara wa gari kumi(10) ambapo kati ya hizo mbili zinakuwa ndogo huku moja ikiwa mbele ya msafara na nyingine ikiwa nyuma ya msafara huku hizo gari zikiwa na alama mahususu kulingana na kemikali iliyobebwa, gari mbili ndogo pia huwa zinabeba wataalam na vifaa tiba ambavyo endapo ajali itatokea vifaa Tiba hivyo vitatumika katika kutoa huduma eneo husika.
Naye Musa Biboze ambaye amemuwakilisha mkurugenzi wa Bandari amesema bandari huwa zinaongezwa na miongozo kutoka kwa mamlaka zinazosimamia bandari Duniani hivyo pia Bandari ya Dar es Salam inatumia miongozo hiyo na miongozo mingine kutoka mamlaka husika hapa nchini.
‘Sisi Bandari ya Dar Es Salaam tunatumia miongozo ya usafirishaji wa kemikali sumu kutoka mamlaka ya Bandari Duniani na mamlaka husika kutoka hapa nchini na tunafuata sheria na taratibu zote’
Amesema Daniel Ndiyo.
Kuhusu usalama uingiaji na utoaji wa mizigo hatarishi katika Bandari ya Dar es salam amesema Bandari kushirikiana na mamlaka zingine zinazohusiana na kemikali ikiwemo mkemia mkuu wa
serikali wanashirikiana vyema na wanafuata taratibu zote za kisheria na kiusalama.
Kwa upande wake Deogratius Chacha ambaye ni mkurugenzi wa masoko na uhusiano wa Umma kutoka kwa Wakala wa Bandari kavu amesema wanawajibika vyema katika kupokea, kuhifadhi mizigo hatarishi, kuwezesha katika ukaguaji na usafirishaji wa mizigo hiyo wanatumia miongozo ya kimataifa na miongozo ya ndani ya nchi inayosimamiwa na mamlaka ya Mkemia mkuu wa serikali na wanafuata namna wanavyoelekezwa na wahusika wakuu.
Kuhusu video inayosambaa mitandao ameshauri Watanzania kuipuza kwani haina ukweli wowote na hamna mizigo yeyote hatarishi inayofunguliwa ndani ya Bandari kavu na kwamba kabla hawajapokea mizigo hiyo hatarishi huwa wanapokea Kwanza kadi za kiusalama ambazo zinatoa maelekezo namna ya mizigo hiyo unavyotakiwa kuhifadhi na kusafirishwa.