Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza Katika kongamano la Baraza la Wanawake Chadema BAWACHA lililofanyika kwenye ukumbu wa Kuringe mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Jana.
Julieth Laizer,Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt.Samia amesema Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe na kutaka amani ijengwe ili mengine yafuate.
Rais Samia ameyasema hayo katika kongamano maalum la wanawake wa Chadema (|Bawacha) lililofanyika mkoani Kilimanjaro.
“Leo hapa tumejawa na furaha, na hiyo ni sababu ya matunda ya mazungumzo ya maridhiano ndugu zangu siasa ni mchezo wa kulumbana kwa hoja…..kasema nini nimzodoe, wote tukiwa na lengo la kushika dola.
“Mimi Dada yenu na wenzangu wanaonisaidia tumefanya ubunifu wa kuhakikisha Taifa hili linaungana na kuwa moja. Tukaviambia vyama vya siasa vikae na kuja na namna wanataka tufanye nini.”
Najua unatandikwa umepewa asali umebadili na ‘tone’, ulipotoka jela ulienda Ikulu mama alikwambia nini? ukienda nje unatandikwa…wahafidhina siku watatuelewa, asante ndugu yangu. (Mbowe) amesema Rais Samia.
Katika hilo chama chenu kikaja na maoni yake ya kutaka kisikilizwe peke yake na mimi nikamwambia Makamu wangu awaite watu wenu watano na upande huu watano mambo yakasonga mbele.”
Baada ya vikao hivyo leo mnamuona Rais amesimama kwenye jukwaa hili kuzungumza na Baraza la Wanawake la CHADEMA, jambo ambalo halikuwa rahisi huko nyuma ila kwa sababu ya ubunifu limewezekana.”
Naye Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amefichua chimbuko la salamu ya ‘no hate, no fear” akieleza kwamba ilibeba ujumbe wakutolipiza kisasi kutokana na yale waliyokuwa wakipitia huko nyuma
Mbowe ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na Baraza la wanawake Chadema(BAWACHA) ambayo yamefanyika kitaifa katika ukumbi wa Kuringe, uliopo katika Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro , ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Mbowe amesema salamu hiyo waliianzisha kwa lengo la kuwapooza Watanzania na wanachama wa chama hicho ili wasiwe ni watu wa kulipiza visasi au kubeba chuki mioyoni mwao.
“Sisi kama chama tulilazimika kufundishana salamu mpya tukafunzana salama inayoitwa “no hate no fear” kwa maumivu na bakora ambazo tulipigwa tulilazimika kubuni salamu ambayo itawapooza wananchi, wanachama wetu, kwamba wasiwe watu wa kulipiza visasi,”
“Na sio watu wa kujenga chuki, ndio tukaanzisha salama ya ‘no hate, no fear, kwamba tuendelee kubaki katika ujasiri wetu lakini tukibaki katika kuogopa kulipa kisasi kwasababu wa kulipiza ni Mungu wetu na wala sio sisi binadamu