Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuongoza kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi wakiwa katika kikao kazi na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara yao na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.
Watumishi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi wakiwa katika kikao kazi na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara yao na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Xavier Daudi
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo kwa watumishi wa Idara ya Uendelezaji Taasisi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.
………………………………….
Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Uendelezaji Taasisi kumpa ushirikiano wa kutosha kwenye eneo la kusimamia uendelezaji wa sera katika Utumishi wa Umma na miundo ya Taasisi za Umma ili aweze kumsaidia vema Waziri mwenye dhamana kufikia lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwa na sera za utumishi wa umma zenye tija na miundo inayotekelezeka kiutendaji kwa ustawi wa taifa.
Mhe. Kikwete ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Usimamizi wa Taasisi kwa nyakati tofauti kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na Idara hizo pamoja na kuhimiza uwajibikaji. Mhe. Kikwete amesema ameteuliwa na Mhe. Rais kumsaidia Waziri mwenye dhamana ya kusimamia utumishi wa umma na utawala bora, hivyo hana budi kufahamu kwa kina majukumu yanayotekelezwa na idara hizo ili aweze kuyazungumzia pale yanapohitaji ufafanuzi na uelewa kwa umma.
“Malengo ya kukutana nanyi leo ni kufahamiana na kujua majukumu yenu kwa kina kwa kuwa mimi nina jukumu la kumsaidia Mhe. Waziri kujibu maswali ya kiutumishi na utawala bora yanayoulizwa Bungeni,” Mhe. Kikwete amesisitiza.
Mhe. Kikwete ameongeza kuwa, anatamani kujua kila kitu
kinachofanyika katika idara hizo pamoja na changamoto
wanazokabiliana nazo kiutendaji kwani kwa kufanya hivyo atakuwa
kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza kwa ufanisi lengo la Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Kikwete ameitaka Idara ya Undelezaji Sera kuhuisha sera za kiutumishi ili ziendane na wakati na ziweke mazingira rafiki ya kuzihusisha sekta binafsi kutoa mchango katika kuboresha utumishi wa umma kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza.
Akimkaribisha Naibu Waziri kuzungumza na watumishi wa Idara ya hizo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema kukutana na Idara hizo kutawawezesha kufahamu kwa kina majukumu yanayotekelezwa na idara hizo ili waweze kusimamia utoaji wa huduma bora kama ilivyokusudiwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tuko kwa ajili ya kujifunza, niwaombe ushirikiano kwani kazi nyingi zinafanywa na ninyi, kwetu sisi ni kukamilisha tu, hivyo mtueleze kipi kinatakiwa kufanyika kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Miongozo ili tufanye yale yaliyokusudiwa kwa maendeleo ya taifa letu,” Katibu Mkuuamesisitiza.Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Katibu Mkuu, Ofisi ya RaisMenejimenti ya Utumishi, Bw. Juma Mkomi wameanza kufanya vikao kazi na watumishi wa Idara na Vitengo vya Ofisi yao
vitakavyowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu mara baada ya kuteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.