Fatuma Mohamed Abdallah Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akijaza mafuta kwenye bajaji ya Sophia Abdallah mwanamke mwenye ulemavu ambaye pia ni dereva wa bajaji jijini Dar es Salaam katika kituocha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka duniani kote.
Fatuma Mohamed Abdallah Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akimkabidhimtungi wa gesi Sophia Abdallah mwanamke mwenye ulemavu ambaye pia ni dereva wa bajaji jijini Dar es Salaam katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka duniani kote.
Fatuma Mohamed Abdallah Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akijaza mafuta kwenye bajaji ya Mariana Mponji mwanamke mwenye ulemavu ambaye pia ni dereva wa bajaji jijini Dar es Salaam katika kituocha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka duniani kote.
Fatuma Mohamed Abdallah Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akimkabidhimtungi wa gesi Sophia Abdallah mwanamke mwenye ulemavu ambaye pia ni dereva wa bajaji jijini Dar es Salaam katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8, kila mwaka duniani kote.
Fatuma Mohamed Abdallah Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania akimsikiliza Bi. Sophia Abdallah mwanamke mwenye ulemavu ambaye pia ni dereva wa bajaji jijini Dar es Salaam wakati akitoa shukurani zake baada ya kupokea zawadi ake katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Puma Energy Upanga jijini Dar es Salaam wakijaza mafuta kwa mmoja wa akina mama waliofika kujaziwa namfuta na kituo hicho.
……………………………………….
Wakati leo Dunia ikiwa inaadhimisha ya siku ya wanawake Kampuni ya Puma Energy Tanzania imetoa mitungi ya gesi pamoja na mafuta kwa wanawake wenye ulemavu ambao ni wapambanaji katika maisha ikiwa ni kuunga mkono na kuitambua siku hii.
Akizungmza na waandishi wa habari Fatuma Mohamed Abdallah ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania amesema kampuni hiyo imeamua kuungana na wanawake ambao wapo katika kundi maalum wenye ulemavu madereva wa Bajaji katika sekta ya usafirishaji kwa kuwaalika ambapo wamewapatiwa mafuta kwenye vyombo vyao vya usafiri pamoja na mitungi ya Gesi kama kuhamasisha wanawake katika matumizi ya nishati safi.
‘Tutagawa mitungi kumi(10) ya kilo sita na tutaungana na wanawake ambao ni madereva wa Bajaji na tutajaza Bajaji zao mafuta’ Amesema Fatuma Mohamed.
Aidha Bi. Fatuma ameongeza kwamba kutoa mitungi kwa akina mama hao pia ni kumuungana mkono Rais Samia suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na janga la uharibifu wa mazingira duniani kote.
‘Sisi Puma tunaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na bei zetu ni nafuu ili kumuwezesha kila mtanzania aweze kutumia gesi katika matumizi ya kupikia’
Hata hivyo kampuni hiyo imrahisisha gharama za manunuzi kwani tayari imeanzisha Application ambayo mtu yeyote anaweza akaitumia kwa kuagiza gesi kupitia Application hiyo na akaletewa hadi nyumbani.
Naye Sophia Abdalla ambaye ni mwanamke mpambanaji Dereva wa Bajaji ametoa shukurani kwa kampuni ya Puma Energy kwa kuwawezesha kuwapa mafuta(‘Full Tank) kwenye bajaji zao na zawadi ya mitungi ya gesi.
‘Nawaamasisha wakina mama wenzangu tupambane katika Biashara ndogo na tutumie Puma Gas kwani ni gesi nzuri yenye viwango vya juu’.