Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uaratibu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (katikati) akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Abubakari Kunenge
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi.
……………………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema wananchi waliotoka katika Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari nakuja kuish katikai Kijiji cha Msomera, sasa wanauwezo wa kumiliki ardhi na Makazi.
Kauli hiyo ameitoa wakati akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika ziara maalumu ya kukabidhi mradi wa uendelezaji wa kijiji cha Msomera kwa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.