Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ,amebainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa pesa kuwawezesha Watanzania kuondoka katika wimbi kubwa la umaskini ikiwa ni kutekeleza malengo ya Milenia
Katika utekelezaji huo amesema Mradi mkubwa wa TASAF umekuwa wa mafanikio kwa walengwa na umewanufaisha kwa wakati
“Tukiwa na mhe Waziri wetu Mhe Jenista Mhagama Tumeon mafanikio makubwa sana ya Mradi wa TASAF katika wilaya ya Siha, Kilimanjaro hii inaonyesha dhahiri dhamira ya Serikali ya kuhakikisha walengwa wananufaika na mradi huu wa TASAF” Alisema Kikwete
Katika ziara hiyo walifika katika kaya ambazo zilieleza jinsi mradi huo unavyowanufaisha walengwa ambapo wameiomba Serikali kuwafikia wananchi wengi zaidi nchini ili kuwasaidia.