…………,…………
Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila mara ili kuimarisha afya ya mwili na akili hali itakayowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi, Prisca Lwangili alipoongoza program ya mazoezi ambayo hufanyika kila siku ya Alhamisi kwa watumishi wa Wizara hiyo.
Mkurugenzi Lwangili, ameongeza kuwa lengo la program hiyo ni kuwapa fursa Watumishi wa Wizara hiyo kufanya mazoezi ikiwa ni mkakati wa kuongeza ufanisi kazini kwa kuwajengea afya njema watumishi hao pamoja na kujenga mshikamano na upendo kazini.
Kufuatia hatua hiyo, Mkurugenzi Lwangili ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara hiyo pamoja Taasisi zake ambazo zipo katika mikoa mingine kuanzisha program hiyo ya mazoezi kwenye maeneo yao ili kila mtumishi aweze kupata nafasi ya kufanya mazoezi.