Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR),Profesa Said Aboud wakati akizungumza katika kongamano la Pili wa Chama cha wataalamu wa vinasaba za binadamu nchini-THGO ambalo limefanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Chama cha Wataalamu wa vinasaba vya binadamu nchini -THGO,Dkt Siana Nkya akizungumza katika kongamano la Pili wa Chama cha wataalamu wa vinasaba za binadamu nchini-THGO ambalo limefanyika leo jijini Dar es salaam
Mjumbe wa Bodi ya THGO na Profesa wa Famasia kutoka kutoka chuo kikuu cha Sayansi na tiba Muhimbili (MUHAS) Raphael Sangeda katika kongamano la Pili wa Chama cha wataalamu wa vinasaba za binadamu nchini-THGO ambalo limefanyika leo jijini Dar es salaam
Baadhi ya washiriki na wataalam kutoka taasisi pamoja na watafiti mbalimbali wa mkutano huo katika kongamano la Pili wa Chama cha wataalamu wa vinasaba za binadamu nchini-THGO ambalo limefanyika leo jijini Dar es salaam.(Picha na Mussa Khalid)
…………………………
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa bado utafiti unahitajika pamoja elimu kwa jamii kuhusu uelewa kuhusu Vinasaba vya binadamu ili kuweza kusaidia katika kufanya matibabu .
Hayo yameeleza jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR),Profesa Said Aboud wakati akizungumza katika kongamano la Pili wa Chama cha wataalamu wa vinasaba za binadamu nchini(THGO) ambao umewakutanisha wataalam kutoka taasisi pamoja na watafiti mbalimbali wenye lengo la kujadili tafiti zinazohusu vinasaba vya binadamu.
Profesa Aboud amesema kuwa tafiti hizo za vinasaba vya binadamu zina umuhimu katika kutambua magonjwa mbalimbali lakini pia katika matumizi ya tiba za magonjwa ambayo mtu anayapata kutokana na kurithi au vinasaba ambavyo amerithi kutoka kwa wazee wake.
‘Tumekutana hapa ili kujadiliana na kubadilishana uzoefu lakini kwa lengo la kuongeza kasi ya matumizi ya kufanya tafiti na matumizi y anjia za kisasa za kutambua vinasaba vya binadamu kwa ajili ya magonjwa na tiba kwani matokeo ya tafiti yanatakiwa kuweza kushawishi katika kufanya maamuzi’amesema Prof Aboud
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalamu wa vinasaba vya binadamu nchini -THGO,Dkt Siana Nkya,amesema lengo la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wa masuala ya afya wenye lengo la kupeana elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu vinasaba vya binadamu.
Dkt Nkya amesema matokeo ya utafiti ya vina saba yataweza kutumika kwa ajili ya dawa za magonjwa yanayopatikana kutokana na vinasaba pamoja na kutumika kwa ajili ya mafunzo.
Naye Mjumbe wa Bodi ya THGO na Profesa wa Famasia kutoka kutoka chuo kikuu cha Sayansi na tiba Muhimbili (MUHAS) Raphael Sangeda ,amesema vinasaba vinaweza kusaidia kutibu magonjwa hivyo ni vyema madaktari wakalitambua hilo.
Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo akiwemo Mwanzilishi wa Tanzania Epilepsei Organisation Fides Peter Uiso pamoja na Yusup Zahoro mmoja ya wahanga wa magonjwa Adimu wameshauri kuongezeka kwa wataalamu ili kusaidia kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Hata hivyo watafiti wametakiwa kufanya utafiti zaidi ili uweze kusaidia katambua magonjwa kwani vinasaba vya binadamu vinaweza kutumika pia kusaidia kutibu magonjwa mbalimbali.