……………………
NA FARIDA MANGUBE MOROGORO
Kuelekea siku ya wanawake Duniani Wazazi wametakiwa kuzingatia malezi kuanzia ngazi ya familia ili kujenga familia imara zenye uwezo wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ikiwemo wazazi kuanza kutenga mda wa kuzungumza na watoto.
wito huo umetolewa na wadau wa maswala ya kijinsia katika kongamano la uunganishaji wa familia kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto uku chanzo kikubwa ikitajwa kuwa ni malezi duni kuanzia ngazi za familia kwani wazazi wamekua hawatengi mda wa kuzungumza na watoto wao na jamii kutakiwa kuhakikisha malezi bora yanaanzia katika ngazi ya familia.
Akizungunza njee ya kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la WICOF Bi Mwajabu Dhahabu alisema familia ndio nguzo katika jamiii hivyo isipokuwa imara inapelekea mmong’onyoka wa maadili
Alisema lengo kuu la kuanzisha Kongamano hilo ni kuwaweka pamoja wazazi na walezi Ili kukumbushana swala Zima la malezi Kwa watoto ambayo Kwa kiasi kiukukwa wazazi wengi wamekuwa wakiwaachia wasaidizi wa nyumbani.
“Siku hizi ukatili umeshamiri kwenye jamii zetu Kila siku vyombo vya habari vinaripoti ukatili lakini chanzo chake ni mmong’onyoka wa maadili unasababishwa na Familia” alisema Bi Mwajabu
Alisema kabla ya kongamano la hilo walishaanza na mangongamano la kuzungumza na vijana pamoja na wanafunzi na kugundua kwamba wazazi wengi hawana muda wa kukaa na watoto wao.
Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Morogoro Faraja Maduhu amewataka wazazi kutumia muda wao kukaa na watoto Ili kujua wanapitia changamoto gani hali itakayosaidia kumaliza ukatili Kwa watoto.
“Tunapoelekea siku ya wanawake Dunia ni vyema tukawapitisha wanawake kwenye maswala ya familia kwani Kwa Sasa jamii inapambana na vitendo visivyoeleka kama mapenzi ya jinsia Moja, Sasa haya mambo yanamtaka Mtoto ajengewe uwezo wa kujiamini na kuwa na ufahamu wa kujiamini na msimamo” alisema Maduhu.