Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Maria Nyoka kushoto,akikabidhi sehemu ya mifuko 40 kati ya 70 ya saruji na mchango kwa mkuu wa shule ya Sekondari Frank weston katika Halmashauri ya wilaya Tunduru mkoani humo ili iweze kutumika kujenga matundu ya vyoo vya shule hiyo.
Mbunge wa viti maalum mkoani Ruvuma Mariam Nyoka,akitengeneza tofali mara baada ya kukabidhi jumla ya mifuko 40 kati 70 ya saruji kwa shule ya Sekondari Frankweston wilayani Tunduru.
Mbunge wa viti maalum mkoani Ruvuma Mariam Nyoka kulia, akichanganya mchanga kwa ajili ya kazi ya kufyatua tofali ili kujenga matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Frankweston wilayani Tunduru.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Frankweston mwishoni mwa wiki alipokwenda katika shule hiyo kukabidhi msaada ya mifuko 70 ya saruji na lori mbili za mchanga ili itumike kujenga matundu ya vyoo vya wavulana.
…………………………………………..
Na Muhidin Amri,
Tunduru
MBUNGE wa viti maalum mkoani Ruvuma Mariam Nyoka,amekabidhi msaada wake wa mifuko 70 ya saruji kwa shule ya Sekondari Frankweston iliyopo kata ya Mlingoti katika Halmashauri ya wilaya Tunduru.
Mifuko hiyo ya saruji itatumika kujenga matundu ya vyoo vipya vya wavulana katika shule hiyo,kufuati vyoo vya hapo awali kubomoka kutokana na mvua kubwa zilizonyesha miezi miwili iliyopita.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa shule hiyo Athanas Bosso,Mbunge Mariam alisema msaada huo ni katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita kuboresha ya sekta ya elimu hapa nchini.
Alisema,akiwa katika ziara yake wilayani Tunduru miezi michache iliyopita,alikukutana na changamoto ya matundu ya vyoo kwenye shule hiyo ambayo amewahi kusoma kuanzia kidato cha 1 hadi 4 na kuguswa na hali hiyo,hivyo ameamua kutoa saruji ili itumike kujenga vyoo vipya.
Alisema,anafahamu kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu Samia Hassan katika kuwaleta maendeleo wananchi kuboresha sekta ya elimu hapa nchini,lakini kama Mbunge wa viti maalum ana wajibu kusaidia kile alichonacho.
“nikuombe sana Mkuu was hue hii kaka yangu Bosso upokee mifuko 40 kati ya 70 na mchango lori mbili ili ziweze kusaidia kumaliza changamoto ya matundu ya vyoo katika shule yetu,naamini saruji hii itaweza kumaliza upungufu wa matundu ya choo kwa wavulana alisema Nyoka.
Aidha,amewaomba watu waliosoma katika shule hiyo hasa wale wenye uwezo wa kifedha,kuisaidia shule ya Frankweston kwa hali na mali ili wanafunzi waliopo waweze kujifunza kutenda wema na kukumbuka kurudisha fadhila watakapokuwa watu wazima.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Athanas Mbosso,amemshukuru Mbunge huyo kwa uaminifu wake ,kutimiza ahadi na mapenzi makubwa kwa shule hiyo kwa kuwaletea saruji ambayo itasaidia kumaliza upungufu wa matundu ya vyoo.
Alisema,upungufu wa matundu ya vyoo katika shule hiyo ni changamoto kubwa kwani wanafunzi 559 wa kike wanatumia matundu 18,hivyo kuwa na upungufu wa matundu 8.
Mbossa alieleza kuwa,kwa upande wa wavulana wako 429 wanaotumia matundu 16 na upungufu ulikuwa matundu 2, lakini baada ya kutitia kwa kwa baadhi ya matundu na kubomoka kwa ukuta changamoto ya matundu imeongezeka.
Huu ni muendelezo wa kutimiza ahadi zake katika wilaya ya Tunduru ambapo kabla ya kutoa saruji hiyo ,amekabidhi magodoro katika Hospitali ya misheni Mbesa,vifaa tiba na shuka Hospitali ya wilaya Tunduru,Baiskeli kwa walemavu na fedha taslimu kwa vikundi mbalimbali vya wanawake na vijana.