Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC Reinhardt Swart, (kulia) akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa
mbio za KiliMarathoni zilizofanyika mkoani Moshi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo kusherehekea miaka 20 ya udhamini
wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa
Meneja Mkuu wa Biashara wa Tanga Cement PLC Peet Brits akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21
waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa
mbio za KiliMarathoni zilizofanyika mkoani Moshi mwishoni mwa wiki ambapo
kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo kusherehekea miaka 20 ya udhamini wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Tanga Cement PLC Mtanga Noor (kulia), akihudumia vinywaji kwa
baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha
maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za KiliMarathoni
zilizofanyika Moshi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo
kusherehekea miaka 20 ya udhamini wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa.
SIMBA Cement imeendelea kuwa kinara wa ufadhili wa mbio za Kilimarathoni kwa miaka 20 sasa huku ikielezwa kuwa mbio hizo za kimataifa zimezidi kuboreka zaidi kila mwaka.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kwa mbio hizo zilizofanyika Februari 26, katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Meneja wa Biashara wa Tanga Cement PLC Peet Brits amesema, huu ni mwaka wa 20 wa ushiriki wao wakiwa wadhamini wakongwe na wakimbiaji kupitia timu za Simba katika mbio hizo ambazo Simba Cement na waandaaji wa Kilimarathoni wamekuwa wakiziboresha hadi kufikia miaka 21 kwa mwaka 2023.
Amesema, udhamini wa mbio hizo ni kutokana na umuhimu wa michezo hasa Kilimarathoni ambayo huwakutanisha wafanyakazi wa Simba Cement na kufanya shughuli hii kwa umoja kama wanavyofanya viwandani pamoja kukutana na wadau pamoja na wateja wao.
“Katika ushiriki wetu hatukuangalia vyeo au nafasi zetu za kazi tuliona, Mkurugenzi Mtendaji akigawa maji kwa wakimbiaji…tulizungumza lugha moja kutoka langoni hadi kileleni kwa ushirikiano na wafanyakazi ambao ni wakimbiaji (Timu Simba,) kwa pamoja na wakimbiaji wengine, wadau na wateja.” Amesema.
Pia amesema, wakati wa baada ya mbio hizo wafanyakazi ambao ni wakimbiaji wamekutana na wateja na wadau wao Kanda ya Kaskazini na kubadilishana mawazo ya uboreshaji katika huduma.
Kuhusiana na mafanikio kupitia mbio za Kilimarathoni Peet amesema, wamefurahi kushirikiana katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya 21 sasa na kufanya vizuri katika mbio hizo pamoja na kutoa huduma ya kugawa maji kwa wakimbiaji wa Kilometa 42 na 21 waliopita katika kituo chao cha kugawa maji.
“Tuna uhakika wakimbiaji wamefurahi kupita katika kituo chetu cha Point 8 wakati wa mbio hizi na kupata huduma, tutaendelea kushiriki katika tukio hili kila mwaka… Tunaipenda na kuithamini Kilimarathoni na tunafurahi kudhamini kwa kugawa maji kwa wateja wetu na wadau wote waliopita katika ‘Water Point’ yetu na hawa ni kutoka katika mikoa ya Kaskazini ikiwemo Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na mikoa mingine.” Ameeleza.
Aidha amesema, kwa mwaka huu walijipanga kufanya vyema zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuongeza idadi ya wakimbiaji kwa timu Simba pamoja na kuongeza nguvu baina yao kwa kuwapa moyo wakimbiaji na kumaliza kwa ushindi.
Vilevile amesema, wamekuwa na Timu hiyo inayojumuisha wafanyakazi si kwa mashindano ya Kilimarathoni pekee na kampuni ilihakikisha gharama zote ikiwemo vifaa, malazi, usafiri na burudani zinatolewa kwa kila mshiriki ili waweze kupata ushindi na kueleza kuwa wamekuwa na mashindano mbalimbali katika idara ambayo yameleta chachu kwa kampuni kudhamini timu hiyo ya Simba.
Peet amesema, kwa mwaka huu mwaka huu wamevenja rekodi kwa kuwa na jumla ya washiriki 28 na kupitia Kilimarathoni wamesherehekea kwa upekee mafanikio ya mwaka 2022 wakiwa washindi wa jumla wa tuzo ya Rais kwa mzalishaji bora wa mwaka na mshindi wa jumla wa tuzo ya taarifa ya fedha iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA.)