………………………..
MOROGORO.
Timu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imetembelea kongano ya uchakataji wa mazao ya chakula (Morogoro Food Processor Clusters Initiative)iliyowezeshwa na COSTECH kupitia miradi hiyo ya kibunifu iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mshauri wa kongano hiyo, Prof. Bendantunguka Tiisekwa amesema kuwa kongano (Cluster) hiyo imekuwa ikijihusisha na utengenezaji wa bidhaa za chakula kama vile unga wa lishe, matunda na mizizi asilia yenye asili ya chakula kama vile soya , muhogo, ulezi, viungo na maziwa kwa kuchakata siagi.
Prof Tiisekwa amefafanua kuwa Kongano hiyo ilianzishwa mwaka 2006 kupitia uwezeshwaji wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Shirika la kuhudumia Viwanda SIDO ikiwa na makampuni machanga 17 uliofadhiliwa na SIDA kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yaliyojikita katika miradi miwili (2) ya unga wa lishe na matunda yaliyokaushwa.
“Kongano hii ni matokeo ya kongano tano (5) zinazofadhiliwa na COSTECH ya uzalishaji wa unga lishe wenye viambata saba (7) yaani ingredients usio na sumu kuvu na umethibitishwa na Shirika la Viwango la Tanzania yaani TBS ” alisisitiza
COSTECH kupitia Sheria namba 7 ya mwaka 1986 Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imekasimiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mshauri Mkuu wa Serikali kwa masuala yote yahusuyo Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) nchini.