NA MUSSA KHALID
Ukiwa unafuatilia muziki wa Reggae Nchini Tanzania katika nyimbo za wasanii mbalimbali huwenda ukawa Jina la Immanuel Marsh hujazoea kulisikia lakini unalolifahamu ni #RAS NONO ambaye ni mmoja ya wasanii ambao kwa sasa anafanya vizuri
nchini kwani amekuwa akiimba kwa mfumo wa mashairi na hivyo kuwafikia wasililizaji kwa ujumbe uliotukuka akilenga kuitafakarisha Jamii kuwa katika mwelekeo chanya.
Ras Nono hivi karibuni amekuwa na muendelezo wa kuibuka na vibao mbalimba ambavyo vimesheheni
jumbe mbalimbali ikiwemo kuwakumbusha watu namna kuwa na miendendo mizuri katika maisha kama utamaduni wa Rastafarai unavyotaka.
Miaka ya Nyumba Ras Nono wakati anaanza harataki za kuimba Muziki wa Reggae nchini aliibuka na vibao kama Sigara Matata ‘Tabasamu Tamu’,’Pwapwapwa’ na ‘Nikamsake’.
Pia nyimbo Nyingine ambazo Ras Nono amezitoa mwa nyakati tofauti ni pamoja na Utulivu,Kundi la JAH,Uumbaji,Babilon Down na In That Day.
Lakini kwa hivi karibuni mwanamuziki wa Huyo wa Reggae Nchini Rasi Nono ameibuka na nyimbo kama ‘Tabia’ ,Penzi Nono’ ,Tafakuri, Lugha,Watu,na Tukuyu ambazo zote mtayarishaji ni Sound Crafters.
“Dhamira yangu ni kuhakikisha ninaimba nyimbo zenye ujumbe ambao hata Mtanzania anaposikiliza ananufaika nao na kuburudika pia kutokana na mashairi yenye kujenga ambayo nitakuwa kila nyimbo yangu nayoitoa ili kuikomboa Jamii
kifikra”amesema Rais NONO
Aidha Nono amesema ameamua kuimba Muziki mzuri kwani ameangalia katika Jamii inahitaji
nini ili kuimba nyimbo ambazo zitakwenda kuwakomboa kifikra Pamoja na kuburudisha na mziki wake.
TUZO.
Mwanzoni mwa Mwezi January Mwaka huu Msanii Huyo wa Muziki wa Reggae Nchini Rasi Nono aliibuka na kunyakua Tuzo ya Mwanamashairi Bora ambazo ziliandaliwa na Taasisi
ya Sanaa ya Kukaye Moto Culture Center ambazo zilifanyila jijini Dar es salaam zikiwa zimesheheni washiriki mbalimbali.
Ras Nono baada ya kupata Tuzo alitumia nafasi hiyo kuipongeza Taasisi hiyo kwa kuona mchango
wake katika tasnia ya Muziki wa Reggae Huku akishauri ziendelee kuwa muendelezo nchini Ili kuonyesha ushirikiano kwa wasanii wa Reggae na Dancehall.
Ras Nono pia amewashauri wasanii nchini kuendelea kufanya muziki mzuri wa Reggae na Dancehall ili kuleta upinzani kwa aina nyingine za miziki na hivyo kuusimamisha
muziki huo
Ras Nono ameendelea kusema kuwa lengo lake ni kuwalenga watu ambao fikra zao zilipotoka na nyimbo zisizokuwa na maadili kwani
wanawaweza kuimba nyimbo za muhimu na zikaishi.